SHARE

Mabao matatu aliyoyafunga dhidi ya klabu ya Bayern Munich yamemfanya Cristiano Ronaldo kufunga jumla ya hat trick 41 ndani ya misimu 8 aliyokuwa Real Madrid ambapo walimchukua toka Manchester United mwaka 2009.

Wakati anajiunga na Real Madrid ilimbidi kusubiri hadi mwaka 2010 ili kupata hat trick yake ya kwanza ambapo ilikuwa katika mchezo wao Real Madrid dhidi ya klabu ya Mallorca katika ligi kuu ya nchini Hispania.

Kabla ya mchezo wa jana, Cristiano Ronaldo alifunga hat trick katika mchezo wa klabu bingwa dunia dhidi ya Kashima Antlers ambapo Madrid walikuwa nyuma kwa magoli 2 kwa 1 kabla Ronaldo kufunga hat trick hiyo na mchezo kuisha kwa 4-1

Lakini hat trick dhidi ya Bayern Munich imemfanya Cristiano Ronaldo kufunga hat trick 6 katika michuano ya champions league, huku 35 zilizobaki akiwa amezifunga kwenye michuano mingine.

Katika kombe la Copa De Rey hadi sasa Cristiano amefunga hat trick mbili, na akiwa amefunga hat trick moja katika kombe la klabu bingwa dunia huku 32 akizifunga katika katika ligi kuu nchini Hispania.

Hat trick dhidi ya Bayern Munich imemfanya Ronaldo kufunga jumla ya mabao 100 katika michuano ya Ulaya na kumfanya kuwa kinara wa ufungaji wa muda wote katika michuano hiyo.

Hadi sasa akiwa na Real Madrid, Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya hat trick nyingi La Liga ikiwa ni jumla ya hat tricks 32, na akifunga mabao 395 katika michezo 386 aliyoitumikia klabu ya Real Madrid.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here