SHARE

Shirika la ndege Turkish Airlines lafahamisha kudhamini masomo ya Kadiju, mtoto aliezaliwa katika ndege ya shirika hilo

Turkish Airlines kumuajiri mtoto aliezaliwa ndani ya ndege yake

Shirika la ndege la Uturuki lafahamisha kudhamini masomo ya Kadiju, mtoto aliezaliwa katika ndege ya shirika hilo

Shirika la ndege la Uturuki la Turkish Airlines lafahamisha kuwa litadhamini masomo ya mtoto aliezaliwa katika ndege yake ikiwa katika safari ya kutokea  Guinea kuelekea Burkina Faso.

Kadiju alizaliwa ndani ya ndege  ya shirika la Turkish Airlines iliokuwa  safarini Aprili 7 mwaka 2017.

Mkurugezi wa shirika la ndege la Uturuki Mehmet İlker Aycı amesema kuwa shirika hilo linataraji kumuona Kadiju akijiunga na shirika pindi atakapo kuwa na umri wa kufanya kazi na kujiunga na shirika hilo.

Hayo mkurugenzi wa shirika hilo  aliyafahamisha kwa waandishi wa habari Alhamis katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Istanbul.

Mkurugenzi Mehmet İlker Aycı alizidi kuafahamisha kuwa shirika la THY lipo tayari kuanza harakati za kuomba uraia wa Uturuki kwa Kadiju ambae mama yake ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Guinea.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here