SHARE

Serikali ya Ankara yakemea vikali shambulizi la kigaidi liliotekelezwa mjini Paris ambapo askari mmoja alifariki.

Mtu alietekeleza shambulizi hilo pia aliuawa na askari waliokuwa wakilinda usalama.

Shambulizi hilo lilitekelezwa karibu na « Champs-Elysée » mjini Paris.

Mshambuliaji huyo alilenga gari la Polisi na kummalizia maisha askari mmoja.

Tangazo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki  limetuma salamu za rambi rambi kwa Ufaransa na familia ya askari aliepoteza maisha.

Tangazo hilo limezidi kufahamisha kuwa Uturuki itazidi kushirikiana na Ufaransa katika kupambana na ugaidi.

Wanamgmbo wa kundi la kigaidi la Daesh wamejinasibu kuhusika na shambulizi hilo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here