SHARE

Miamba wa soka wa Marekani,LA Galaxy wametangaza rasmi kuachana na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Manchester United,Zlatan Ibrahimovic.
LA Galaxy wameamua kuachana na Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 36 baada ya mshambuliaji huyo za zamani wa Paris Saint Germain kupata jeraha la goti ambalo litamweka nje ya dimba kwa muda wa miezi tisa.
Na sasa LA Galaxy wamegeukia mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa,Andre Pierre Gignac anayekipiga Tigres ya Mexico.
Gignac mwenye umri wa miaka 31 ameingia kwenye rada za miamba hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani baada ya kuifungia Tigers mabao 44 katika michezo 71.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here