SHARE

MTUNZI: FRANK DAVID.
CONTACT: 0769510060.
TITTLE: SIRUDI NYUMBANI.
SEHEMU YA KWANZA
Naitwa Vedasto mtoto wa pekee katika familia ya mzee James. Mimi sikuwa na bahati kabisa ya kulelewa na wazazi wote wawili yaani baba pamoja na mama, ila nilibahatika kulelewa na mama tu, na hii yote ilikuwa ni kwasababu baba na mama walishindwa kuishi wote pamoja, maana baba mzazi alimfumania mama yangu na mwanaume mwingine, hivyo baba alimfukuza mama na alinikataa ata mimi na kunikana kabisa akisema hajanizaa yeye, maana baba alihisi mama ata mimba yangu aliipata kupitia uzinzi wake na kumsingizia yeye, hivyo tulifukuzwa wote mimi pamoja na mama, kipindi hicho nilikuwa mdogo sana na wala sikuwa na uwezo wowote wa kumsaidia mama yangu kwa lolote lile.
Baba alimshangaa sana mama, maana kipindi anamfukuza pale nyumbani alihisi labda mama atalia na kuomba msamaa ila mama alisema, “mme wangu naondoka lakini huyu mtoto ni damu yako” kweli tuliondoka kutoka nyumbani na kumuacha baba peke yake. Mama alipangishiwa chumba na Yule hawara yake, hivyo tukawa tunaishi vizuri tu, ila baada ya kama mwaka mmoja Yule hawara yake mama akawa ameugua sana mpaka akafariki, na kibaya zaidi alimuacha mama na ujauzito wa wiki 2 alafu kipindi hicho mama alikuwa hana kazi wala msaada wowote ule maana mama alikuwa sio mtu wa kujishughulisha bali yeye alikuwa akiamka asubuhi anaoga na kukaa sebreni kuangalia TV kishaYule hawara yake akija anatoa hela ya matumizi na maisha yanaenda tu.
Sasa hawara alipo fariki mambo yalibadilika sana kwasababu mama yangu hakuwa tena na njia yoyote ya kupata pesa na ukiangalia upande wa pili mama hakuwa na kazi yoyote, hivyo ikafika hatua tukaanza kula mlo mmoja tu kwa siku mimi pamoja na mama yangu.
Baada ya mda kodi ya nyumba ambayo mama alikuwa amepangishiwa na hawara yake ikaisha na mwenye nyumba alikuwa mtata kwelikweli yaani yeye kodi ikiisha hataki masihara bali anataka pesa tu, Yule bibi mwenye ile nyumba akamfata mama,
“habari mpangaji wangu nimekuletea taarifa kuwa mda wako wa kukaa hapa umekwisha, hivyo unatakiwa kulipia kodi upya au kama huwezi kulipa ni ruksa kuachia chumba” alisema mama mwenye nyumba,
“naomba univumilie mama yangu ndani ya hizi wiki mbili maana sahivi sina pesa, mme wangu alifariki hivyo nina matatizo sahivi” alisema mama.
“we we wehh, mimi sina masiahara ya nyumba yangu, yaani kuhusu kusaidia ni bora nikupe pesa lakini nyumba yangu kuifanyia masihara sipendi kabisaaa, huwezi kukaa wiki mbili hapa kwangu bure, ila kwasababu umepatwa na matatizo maana bwana yako alifariki nakupa siku tano tu uwe umeleta pesa yangu laki tatu na sitini” alisema mama mwenye nyumba kisha akatoka nje akiwa amenuna.
Mama yangu alianza kulia na kujutia kwanini tamaa za mwili zilisababisha amuache baba yangu mzazi, ndipo mama akapata wazo la kurudi nyumbani kwa baba yangu ili aombe msamaa waweze kurudiana na kuanza maisha mapya, ila mama alipo fika kwa baba akashangaa kuona anakaribishwa na mwanamke mwingine ambae ni mpole na mstaarabu sana aitwae Bhoke wakaanza kuongea na mama.
Bhoke, “karibu dada maana tangu umefika hapa naona upo kimya alafu mimi sikujui ningependa tutambulishane”
Mama, “ mimi ndiyo ningependa kukufahamu wewe maana nimekukuta kwangu, hapa ni kwa mme wangu na huyu mtoto na wa mwenye hii nyumba”
Bhoke, “we dada nahisi umepotea njia naomba utoke kwangu, mimi ndiyo nimeolewa hapa na mme wangu hayupo sahivi ameenda kazini, nahisi umekosea njia rafiki yangu, kaangalie nyumba zingine sio hapa”
Mama yangu aliamka na kwenda mpaka chumbani kwa baba kisha akalala kitandani akasema “kitanda hichi nilikinunua mimi pamoja na mme wangu, ata hili shuka pia nimelinunua mwenyewe sokoni sasa nashangaa unajifanya mjuaji” .
Bhoke alianza kulia maana alikuwa mpole sana yule dada na alikuwa mrembo sanaaa binti wa kikurya na baba alimuoa baada ya kumfumania mama na hawara yake, Bhoke akaamua tu kukaa malangoni hasira zikiwa zimempanda mno anashindwa afanye nini kwa mama.
Baada ya masaa kadhaa baba akawa ame wasili kutoka kazini, akashangaa kukuta mke wake yaani bhoke macho yamevimba na yamekuwa mekunduu maana alilia sana siku hiyo.
Baba akamuuliza “unalia nini,”
Bhoke akajibu “kuna mke wako huko chumbani, sasa sijui ulinioa na kunitolea mahari ili uje kunidhalilisha, naomba tu unirudishe nyumbani kwetu Musoma siwezi kukaa ni huyo mwanamke humu ndani,”
Baba akaenda chumbani kwake haraka haraka, kabla hajafika vizuri akajikwaa na kudondoka chini ila akaamka tena kisha akaingia chumbani, alipo tazama kitandani akakuta mtu na mtoto wamelala huku wakiwa wamejifunika shuka mpaka usoni, ndipo baba akasogea polepole mpaka kitandani kisha akashika lile shuka na kulivuta, mama alikuwa amelala kifudifudi hivyo hakuweza kumuona alie mfunua kwa haraka, ndipo mama akatamka maneno machafu bila kuangalia alie mfunua kwamba, “hivi wewe changudoa, sinimekwambia haya mashuka niliyanunua mimi sokoni, sasa kwanini unanifunua, nimesema usiniamshe kichaa changu nitakupiga mpaka usahau njia ya kwenda kwenu” kisha akasonya.
Mama alitukana vile akihisi anamwambia Bhoke, kumbe anamwambia baba, Daaaah baba alichukia sana kisha akasema, “hivi we mwanamke una akili kweli wewe, yaani umetoka huko kote na kuja kunivurugia ndoa yangu, hivi we unajua mke wangu nilipo mtoa, nakuomba we Malaya toka nje ya nyumba yangu, ulikuwa na tamaa na wanaume nenda uwafate huko huko, na ukirudi tena hapa, ehhh sikia aki ya mungu nakuua”
Baba alimfukuza mama kwa hasira sana, kipindi anamsukum mimi nipo tu ila bado mdogo bado nalia tu siwezi kutetea chochote na ndiyo nilikuwa nimeanza kujua kutembea, nilianguka chini vibaya nikaumia kichwani ila baba hakuwa na huruma tulifukuzwa kama wezi, ndipo bhoke akapata tabasamu usoni mwake maana siku yake ilikuwa mbaya sana kipindi mme wake hajafika.
Mama mwenye nyumba hakutaka masiala kabisaaa akamwambia mama kwamba naona huruma imezidi sasa nakupa wiki moja tu usipo toa hela, vitu vyako unavikuta nje, kama umekosa pesa kauze ata mwili wako, mi mwenyewe hii nyumba nimeijenga kwa tabu sana kipindi nina umri mdogo kama wako, tafuta bwana mchune lipa kodi acha kuzubaa mungu kakupa mvuto utumie vizuri.
Kweli mama akaanza tabia za ajabu sana, maana alikuwa anabadilisha sana wanaume kusudi apate pesa ili mimi na yeye tupate kula na kulipia kodi, mama mwenye nyumba alimpenda mama maana alianza kumlipa vizuri tu, maisha yaliendelea mama akiwa anaendelea na biashara zake za kujiuza ili akidhi maitaji yake. Siku moja usiku mama alipatwa na maumivu makali sana mwilini mwake tumbo lilimuuma sana alafu damu nzito nzito zilianza kuvuja kupitia sehemu nyeti, mama alipatwa na maumivu sana hadi huruma ukimtazama, kumbe mama alikuwa amemeza dawa za kutoa mimba ambayo alikuwa ameachiwa na hawara yake, maana alijua kabisa akipata ujauzito itakuwa ngumu kufanya biashara yake ya kujiuza maana hatopata wateja wakimuona na tumbo kubwa, mama aliangaika sana siku ile ndipo mama mwenye nyumba akampeleka hospitali.
Mama aligombezwa sana na daktari kwa kile kitendo alicho fanya cha kutoa mimba ila mama alimwamba kwamba, “daktari mimi sina mme sina kazi, mme wangu amefariki na kuniachia hii mimba mimi nitailea vipi sasa ndiyo maana nimeitoa tu” daktali akasema “futa machozi sasa usilie”
Mama alipona vizuri tu na maisha yakaendelea kama kawaida, baada ya miaka kadhaa nilianzishwa shule ya msingi ila sikusoma chekechea, na mama alifanya vile ili mida ambayo nitakuwa shuleni, wale wateja wake wa mchana au asubui aweze kuwaleta chumbani kwake maana alijua fika mimi nipo shule na hakupenda kabisa kufanya ngono mbele ya macho yangu.
Siku moja tukiwa shuleni mida ya saa mbili asubui, siku ya alhamisi, kengele iligongwa tulishangaa wote maana iligongwa mapema sana tukatoka wote na kwenda kumsikiliza mwalimu mkuu, ndipo tulipata taarifa mbaya maana mwalimu Husna wa somo la Kiswahili wa darasa la 5B alikuwa amefariki hivyo tukatawanyishwa wote mapema ila baadhi ya wanafunzi wa darasa la 5 mpaka la 7 wakaenda kwenye msiba
Mimi nikaamua kurudi nyumbani mda huohuo, kumbe mama yangu mzazi alikuwa yumo ndani na mwanaume wanazini mda huo pia, na mama alipenda kufanyia hilo tendo ndani kwake maana alikuwa akiingiza mwanaume ndani anapata faida kubwa sababu analipwa na pesa ya chumba pia. Sasa kibaya zaidi walijisahau ata kubana mlango, na mimi nilikuwa nakuja haraka ili nibadirishe nguo za shule nikacheze, nilipo fika mlangoni nikaufungua na kuingia ndani dahhhh sikuamini macho yangu kabisa ndipo mama akasema……………………………………….USIKOSE SEHEMU YA PILI.
MTUNZI: FRANK DAVID……………………………………..CONTACT: +255769510060


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here