SHARE

MTUNZI: FRANK DAVID
TITTLE: SIRUDI NYUMBANI
POWERED BY: HADITHIZETU
WHATSAPP: 0769510060
SEHEMU YA NNE.
Kipindi tupo kituo cha polisi hatujui ili wala lile, kwa upande wangu niliumia sana maana niliona ni bora ningekamatwa mimi mwenyewe na sio mama yangu,na yote hayo ilikuwa ni sababu ya umasikini wetu, maana kama kweli mama yangu angekuwa na pesa basi isingewezekana yeye na mimi wote kukamatwa, kiukweli nilijuta sana kujuana na queen, maana nafsi ilinichoma sana kila saa na dakika zilipo kuwa zikienda mbele, kwa sababu sikuweza kutambua nini hatima yangu na mama yangu kuwepo pale polisi.
Sasa kibaya zaidi ni kwamba umri wa mama yangu ulikuwa ni mdogo pia mama hakuwa mzee, hivyo kipindi yupo mule mahabusu amefungiwa ndani akiwa anawaza atatoka vipi pale polisi na ndiyo siku hiyo hiyo alikuwa anaingia hedhi na ilikuwa ngumu sana kupata pedi, hivyo mama akaamua kuvumilia tu. Baada ya wiki moja kupita tukiwa ndani, tukiwa hatujaoga wala kula chakula kizuri, zaidi ya kula ugali ambao haujaiva vizuri na mboga mbaya na bila kunawa ata mikono, baba yangu mzazi alie mfukuza mama yangu kipindi nikiwa mdogo akaamua kufanya mpango wa kututoa polisi.
Mkuu wa kituo alikataa katakata kutuachia, baba alibembeleza sana ila ilikuwa ngumu kutoka, na kingine ni kwamba tayari baba queen alikuwa ametoa rushwa hivyo ilikuwa ngumu kwetu sisi kutoka nje ya pale na kuachiwa huru, ndipo baba yangu akaamua kwenda mpaka kwenye familia ya baba yake queen ili atuombee msamaa, alipo fika kwake alishangaa sana kumuona baba queen maana alisoma nae elimu ya sekondari na walikuwa wamepotezana miaka mingi sana, isitoshe kipindi wapo shule walikuwa marafiki mno hivyo baba queen akawa mpole na hiyo ndiyo ikawa pona pona yetu sisi kutoka mule polisi.
Baba queen alichukia sana kutuona tukitoka na alisikitika pia kuona kwamba familia masikini kama yetu inamvurugia familia yake ila hakuwa na jinsi, lakini alinionya sana na akasema nikae mbali sana na familia yake kilicho nikwaza ni pale alipo sema nisithubutu kumsogelea mtoto ata kama akizaliwa sio mali yangu.
Baba yangu akamwambia mama kwamba, “mama Vedsto hivi kwanini unamlea mtoto wetu vibaya, angalia sasa amebebesha mtoto wa mtu mimba, hivi bila mimi kujuana na Yule baba mnazani mngetoka polisi, mngefia jela nyie nakwambia ukweli”, mama akasema, “yaani huyu kijana mimi sielewi kabisa kwanini kafanya hivyo, maana mimi namuona ni mpole kweli, sikutegemea kama angefanya tabia kama hiyo”, baba alichukia sana akanivuta kisha akanifinya kweli kweli.
Baada ya miezi kadhaa matokeo ya kidato cha nne yalitoka ila kwa bahati mbaya wote mimi pamoja na queen tulifeli tukapata ziro kabisaaa, na hii yote ilisababishwa na matatizo yaliyo tukuta kipindi queen amezidiwa wakati tukilazimisha kutoa mimba.
Wazazi wa queen walichachamaa sana hususan mama queen akasema “binti yangu queen umenikera sana kwa hiyo ziro yako shuleni,yaani sikia queen, kupata mimba nikawaida na sikukugombeza sana alie chukia sana ni baba yako, na mimi nilinyamaza nilivyo gundua una mimba, maana ata mimi marehemu mtoto wangu wa kwanza nilibebeshwa mimba yake nikiwa bado nipo shule, ila mimi sikupata ziro kwenye matokeo yangu, sasa wewe mimba umepewa matokeo yako ni ziro ata cheti hupati hii aibu tunaipeleka wapi sisi. Haya huyo mwanaume mwenyewe aliekupa mimba nae mbumbumbu tu kapata ziro pia, sasa nyie mtaishi vipi sasa, au atakama kuwasaidia tutawasaidiaje sisi”
Baba queen akasema, “mke wangu yaani ili litoto lako ni bora tungezaa vitunguu labda vingetusaida kuhungia mboga na kachumbari ila sio hii hasara, gharama zote zimekwenda burebure, marafiki zake wote wale kina Hellen, Linda, Zubeda, Asha na Yule Maria wa kule sokoni wamefaulu wote ila yeye kapata ziro, atabaki ndani hapa na kazi zote za ndani atafanya yeye humu sialibu pesa zangu tena naapa kwajina la mungu”
Mama queen akadakia kwamba, “mme wangu usiseme hivyo, kumbuka matatizo tumeumbiwa sisi binadamu, mtoto wetu kateleza kidogo tu, na ninazani kwa matatizo haya awezi tena kurudia kosa tumsamee queen mme wangu ebu mtazame anavyo lia anakosa raha mda wote na kibaya zaidi ni mjamzito anaweza kupata matatizo juu ya matatizo tukampoteza” .
“ haya sawa nimekuelewa mke wangu tusahau yote yaliyo pita tuangalie jinsi ya kumsaidia mtoto” alijibu baba queen. Baada ya miezi kadhaa kipindi mimi bado naendelea kukaa na mama yangu taarifa zilitufikia kuwa, queen amejifungua mtoto mzuri wa kiume na anafanana na mimi sana, hivyo mimi kwa upande wangu nilikuwa na hamu sana ya kumuona mwanangu, sikuoga siku hiyo sema kweli, nilivaa suruali haraka haraka na kukimbia kwenye hospitali aliyo kuwepo, ila kwa bahati mbaya nikakuta wameisha toka, ndipo nikaamua kwenda mpaka nyumbani kwa kina queen kusudi niweze kumuona mwanangu.
Nilipo fika nikakalibishwa ndani, wakati nimekaa sina habari baba queen alikuja akiwa na mbwa wake wa kizungu mkubwaaa yaani ukimtazama Yule mbwa unaweza kuogopa maana anaweza ata kumtafuna mtu. Baba queen akasema, “kijana sinilikwambia ukae mbali na binti yangu, na nikasema mtoto akizaliwa hakuhusu” nikajibu, “ndiyo” akasema “sasa umefata nini kwangu, unataka uwe halali ya mbwa wangu, nimruhusu akung`ate” nikasema “hapana baba nilikuja tu kumuona mtoto wangu, naomba unisamee” baba queen akasema “wewe bado mtoto mdogo sana, sitaki ufe ebu toka kwangu, kabla sijachukia mimi” ndipo na mimi nikaamua kutoka na kuondoka.
Nilipo ondoka kumbe kile kitendo kilimkwaza sana mama queen akasema, “mme wangu umefanya kosa kubwa kumfukuza Yule kijana, ni bora ungemruhusu amuone mtoto wake, maana bila yeye tusinge mpata huyu mjukuu”,
“mke wangu unapo elekea tutagombana sana, yaani wewe unatetea mtu kama Yule, achana nae huyo angalia maisha yetu mama queen” alisema baba queen.
Nilipo fika nyumbani nikamkuta mama anapika, akaniuliza, “mwanangu vipi mzazi anaendeleaje,” kabla sijamjibu machozi yakanidondoka, mama akasema “vipi vedasto mwanangu mbona unaniogopesha au hajajifungua salama tumedanganywa”
Nilimjibu nikiwa nalia kwamba, “baba yake queen kanifukuza kama mwizi, akisema nisimtambue mtoto, na ata siku bahatika kumuona mtoto wangu anavyo fanana” mama aliumia sana pia akasema usijali mwanangu, najua haya yote ni sababu ya umasikini wetu ila ipo siku wataona umuhimu wetu”
Nilikosa raha mda wote nikahisi dunia yote ni chungu maana ata masomo yangu nilifeli sababu ya huohuo ujauzito alafu mtoto anazaliwa wananinyima ata kumuona tu, nilimchukia pia queen maana nilimuona ni binti asie kuwa na msimamo, maana aliwasikiliza tu wazazi wake badala ya kunitetea tumlee mtoto pamoja yeye akakaa kimya.
Niliamua kwenda ustawi wa jamii kusudi niweze kuwapa malalamishi kwanini sitakiwi kumuona mwanangu wa damu, lakini baba queen alitumia hela zake mpaka sikufanikisha kabisa kila njia zangu.
Siku moja usiku nikiwa nawaza sana kwanini umasikini unasababisha nisimpate mwanangu, ndipo nikapata wazo la kwenda kwa Yule bibi alie mtibu queen kipindi akiwa amezidiwa na mimba yake tulipo kuwa tunaitoa, nilipo fika kwake nikamuelezea hari halisi, Yule bibi alikasilika sana akasema, “hivi wazazi wake mbona wana roho mbaya sana, hawajui jinsi ulivyo angaika nae mpaka akawa salama, na hawajui huyo mtoto bila wewe asinge zaliwa, sasa ngoja utaona mpenzi wako lazima aje na mtaishi wote.
Bibi alinipa dawa za mitishamba kisha akasema niziweke kwenye chai kila ninapo kunywa, na nilitaje jina la queen kila ninapo kunywa mpaka chai inaisha kwenye kikombe, na hapo ndipo queen mda wote atakuwa ananiwaza mimi na hatoweza kufanya chochote mpaka anione mimi.
Nilifanya hivyo kama wiki nzima bila mafanikio yoyote mpaka nikahisi Yule bibi ni muongo, lakini siku moja nilishangaa queen amekuja nyumbani na mtoto akiwa amemshikilia mikononi kisha akasema, ‘Vedasto bado nakupenda sana mpenzi wangu, ila baba anataka kunisafirisha nje ya nchi na anataka nitoroke na mtoto wako, ila nimetoroka nyumbani na mtoto nimekuletea wewe hivyo mtunze vizuri na salama na mungu akipenda tutaonana,
Sikuamini macho yangu nilipo kabidhiwa mwanangu ndipo nikambusu shavuni queen pamoja na mwanangu alafu nikampeleka ndani, queen akarudi kwao, sasa baba queen alipo rudi kutoka kazini kwake akauliza, “queen, mjukuu wangu yuko wapi mbona simuoni” queen akawa kama hajielewi maana ni dawa za Yule bibi zilisababisha mpaka akamleta mtoto kwangu, kipindi hicho mimi na mama yangu tunamuogesha mtoto na tuna mnywesha mziwa pale nyumbani. Baba queen akauliza tena “queen binti yangu mbona leo simuoni mjukuu yuko wapi?” queen akaanza kuumwa tumbo la uzazi mpaka akaanza kujigaragaza chini akiitaji mwanae arudi, na kipindi hicho pia baba yake hajui mtoto yuko wapi na mama queen naye hayupo.
Baba queen akasema, “binti yangu mbona huongei unajigaragaza chini tu, sikuelewi”, queen alilia sana maana alikuwa kama anahisi kunakitu kinamvuruga kichwani ambacho ata akiwezi kutambulika, isitoshe tumbo la uzazi pia lilikuwa linamuuma sana, alipo pata nguvu kidogo akasema “mtoto yupo kwa vedasto” baba queen hakuchelewa hapo hapo akaja nyumbani, alipo fika hakutaka kuongea akamchukua mtoto na kumrudisha kwao. Ndipo queen akaacha kusumbuliwa na vitu vya ajabu akilini mwake na tumbo pia likaacha kuuma.
Sasa siku moja usiku wakiwa wamelala wote nyumbani milango ikiwa imefungwa, baba queen alishangaa sana kusikia sauti ya mtoto inalia nje ya nyumba tena kibaya mlangoni kwa nje, ndipo baba queen akatoka nje haraka, alipo fika akashangaa mtoto anae lia ni mjukuu wake, akajiuliza imekuwaje mtoto analala nje hapa kwenye mbu kwani huyu queen ameshindwa kabisa kulala na mtoto wake, akaenda kuangalia chumbani kwa queen kama kuna mtoto ila chakushangaza akakuta mtoto yupo na queen tena wamelala bila wasiwasi, baba queen aliogopa akarudi chumbani kwake kulala tu.
Sasa kutokana na ile hali aliyo mtokea baba queen usiku akawa ameogopa hivyo kuna watu walimshauri kuwa, huo utakuwa ushirikina hivyo angemsafirisha binti mapema aende kwa ndugu zake uko Marekani na amtoe huku Tanzania.
Sasa kwa upande wangu mimi baba queen alipo mchukua mtoto niliishiwa nguvu sana,hivyo nikapanga kwamba, nije kumuiba mwanangu alafu niame mji kabisa niende nae mbali wakitutafuta wasitupate kabisa, sasa kipindi napanga vile kumbe na queen kesho yake anasafirishwa kwenda marekani bila mimi kuwa na taarifa, na kibaya zaidi alikuwa anaenda na mtoto wangu. Nilikuja kugundua kuwa queen anasafirishwa baada ya kuambiwa na watu kuwa queen anaenda uwanja wa ndege hivyo niende kusudi nimuage mtoto wangu kwa mala ya mwisho maana sitoweza kumuona tena.
Baada ya kupata taarifa ile niliwai sana uwanja wa ndege kusudi nimchukue mwanangu kwa vita na uvumbi maana niliona zile ni kama dharau, ila niliumia sana jamani, maana wakati nafika tu na ndege nayo ilikuwa inapaa kuondoka, hivyo mtoto wangu sikuweza kumuona tena na queen akawa amesafilishwa pia, niliumia sana moyoni nikatamani ata kufa ila mama akanikalisha chini na kunipa moyo, familia ya kina queen niliichukia sana, kipindi sasa queen amefika marekani akampigia baba yake simu na kumwambia kwamba…USIKOSE SEHEMU YA TANO
MTUNZI: FRANK DAVID, daktari wa hadithi TZ
WHTSAPP: 0769510060
POWERED BY @HADITHIZETU
MITANDAO YOTE YA KIJAMII= @HADITHIZETU


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here