SHARE
Mkuu wa kitengo cha Masoko na mahusiano ya Benki ya Biashara ya TIB Corporate , Theresia Soka akizungumzia ubora wa huduma hizo..

Katika kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli benki ya biashara ya TIB  imeanzisha huduma za kibenki kwa masaa 24 katika tawi dogo la benki hiyo lililopo katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya TIB Corporate Frank Nyabundege, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya benki hiyo kufanya kazi saa 24 Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya  TIB Frank Nyabundege amesema huduma hiyo inawawezesha wananchi wote  kulipia kodi za aina mbali mbali pamoja na tozo zote za bandari.

Amesema hivi karibuni TIB benki na TRA ziliingia mkataba kwa  kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ambapo mtu akilipa kodi kupitia mfumo huo katika tawi lolote la benki hiyo, taarifa zake zitaonekana  moja kwa moja kwenye mtandao wa TRA.

Amesema kuwa, benki hiyo ya biashara (TIB), ndiyo benki pekee yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za TPA hivyo mwananchi atakapolipia tozo yoyote  bandarini taarifa zake huonekana mara moja katika mtandao wake hivyo kurahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine za utoaji mizigo
kwa haraka zaidi.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na mahusiano ya Benki ya Biashara ya TIB Corporate , Theresia Soka akizungumzia ubora wa huduma hizo.

“TIB bank inatoa huduma mbali mbali kutokana na mahitaji ya mteja, zikiwemo za akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya muda mfupi na muda wa kati dhamana za  kibenki uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni na shughuli zote za  kibenki”, amesema Nyabundege.

Aidha amesema, benki hiyo ya kibiashara yenye matawi 6 nchini, Dar es Salaam matatu, Mwanza, Arusha na Mbeya inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na pia inatoa huduma kwa watu binafsi taasisi binafsi na serikali.

Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya TIB Corporate wakifuatilia Mkutano huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here