SHARE

Kampuni ya simu ya Mkononi ya itel imemtambulisha Msanii Bongo Movie, Irene Uwoya kuwa Balozi wa kampuni hiyo hapa nchini.

Mkuruegenzi wa itel, Coopeer Chan akisaini makubaliano na Msanii Bongo Movie, Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Irene amesema amejisikia faraja kuwa balozi na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu.

Amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na kuweza kufanya makubaliano ya kuwa balozi katika kuunganisha itel na watanzania  kwa ujumla.

Kwa upande  Mkurugenzi wa itel, Coopeer Chan amesema kuwa wanatarajia  jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Irene Uwoya katika matukio ya kuonyesha ukarimu kwa baadhi ya makundi kwa utoaji wa misaada.

Amesema kuwa wanamkaribisha balozi mpya itel Tanzania Irene Uwoya kuungana na familia ya kubwa ya itel.

“Sote tunafahamu mchango wa Irene Uwoya kwenye jamii amekuwa akielimisha kupitia filamu zake na kutambua umuhimu wake sisi itel Mobile tutashirikiana naye kikamilifu kuhakikisha jamii inapata kile inachotarajia kukipata kwetu na kwake pia”  amesema Chan.

Msanii Bongo Movie ,Irene Uwoya akizungumza na waandishi wa habari juu kuwa balozi wa Kampuni ya Simu ya Mkononi leo jijini Dar es Salaam.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here