SHARE
Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tecno,, Erick Mkomoye akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika ukumbi huo.

Kampuni ya simu za  mkononi ya Tecno  imeandaa tafrija fupi iliyowakutanisha pamoja wateja wa simu za Tecno, wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wauzaji wa simu kwa jumla.

Meneja Mahusiano wa kampuni ya Tecno Tanzania Eric Mkomoye akiongea na waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es salaam

Tafrija hiyo iliyofanyika Jumamosi jioni katika ukumbi wa  Dar Free Market jijini Dar es salaam na kupewa zawadi ya tiketi kwa wateja zaidi ya 170 kuweza kuangalia movie mpya kabisa katika ukumbi wa Century Cinemax.

Akiongea na waandishi wa habari meneja mahusiano wa kampuni hiyo Eric Mkomoye alisema kuwa mara kwa mara Tecno imekuwa ikitoa zawadi kwa wateja wake. Hii ikiwa na lengo la kuwakutanisha pamoja na kuwa karibu na wateja wao ili kujua matatizo na changamoto wanazokuna nazo wateja wao.

Mkomoye kusisitiza kuwa kuna simu mpya kwa sasa inayoitwa Camon CX ambayo inafanya vizuri sokoni na ina ubora wa hali ya juu wakupiga picha na mega pix 16 kwa kila camera ya mbele na nyuma na ina flash 2 kwenye camera ya mbele na 4 camera ya nyuma.

Balozi wa simu za Tecno nchini Tony Albert (TBWAY) akizungumza na wana habari juu ya uzuri wa simu mpya ya Tecno CX kwa waandishi wa habari.
Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Tecno,, Erick Mkomoye akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika ukumbi huo.
Baadhi ya wadau wa Tecno wakisheherekea na Selfie ya Tecno Camon CX.
Afisa huduma kwa wateja Christina Simbano akikabidhi tiketi kwa mshindi wa kuingia sinema Christina Christopher

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here