SHARE

Mwenge wa Uhuru upo Jijini Dar es Salaam kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo siku ya leo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi amekabidhiwa Mwenge huo ukitokea Wilaya ya Ilala.

Katika miradi tisa ya maendeleo ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kionondoni, mradi wa WOISO ni mmoja wapo, mradi huu upo maeneo ya Salasala chini ya kiwanda cha WOISO ORIGINAL PRODUCT na umejikita zaidi katika utengenezaji waViatu Vya Shule, Mabegi ya shule na ya kusafiria, Mikanda ya Suruali Majaketi ya mvua na baridi, Viatu vya wazi , Masofa na Viatu vya Jeshi ‘Army Boot’.

Mradi huu chini ya juhudi za mzawa WOISO zimepelekea idadi kubwa ya watanzania kupata ajira ambapo inakadiriwa wanawake 136 na wanaume 88 sawa na idadi ya watu 224 wamepata ajira katika kiwanda hicho.

Juhudi hizo za Mtanzania WOISO za kuiunga Mkono Serikali ya Awamu ya Tano kwa kukuza uchumi kupitia viwanda zimepelekea Mkuu wa Msafara wa Mwenge Ahmed Amour amepongeza jitihada hizo zenye malengo chanya kwa maendeleo ya Taifa, na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli na kuwataka watanzania wengine waige mfano huo ili Tanzania ya viwanda ifikiwe.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here