SHARE

 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amur amezindua miradi ya biioni 2.8 katika wilaya ya ubungo jana ikiwemo kituo cha mabasi Simu 2000 na kuwataka askari polisi kufanya ukaguzi katika kituo hicho kwa abiria wanaoingia na kutoka ili kuweza kudhibiti uingizwaji wa madawa ya kulevya na kukamata madereva wanaovunja sheria ili kulinda afya ya watanzania wengi.

Akihotubia wananchi kiongozi huyo alisema madereva wanatakiwa kufuata alama za barabarani na kuacha kupakiza abiria kwa kuzidisha kiwango ili kuepuka ajari zisizo za lazima nchini.

Amour aliwataka madereva kuacha kukwepa  kulipa kodi kwani ni kosa na kusababisha kuikosesha serikali mapato mengi na kuwataka wafuate sheria zote na kuwataka wakitunze kituo hicho haswa kwa kuzingatia usafi ili kiweze kuwa bora zaidi.

Mwenge huo wa uhuru ambao umezingatia kuamasisha wananchi kujari bidhaa za nyumbani na kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa kama maralia na ukimwi amewataka wananchi kujali afya zao kwa kupinga maambukizi yasiyo ya lazima na kuwataka Watanzania kununua bidhaa za nyumbani ili kukuza Tanzania ya viwanda.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here