SHARE

Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya kampuni ya Richmond na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amewataka watanzania kumuacha Rais Dkt. Magufuli kuendelea kupitisha fagio sehemu mbalimbali kwani nchi ilipokuwa imefikia ni pabaya.

Lowassa amesema kuwa ni kweli kuna baadhi ya mambo anakosea lakini si wakati wake kumkosoa kwa sasa hivyo watanzania wanatakiwa wamuunge mkono kwa kile anachokifanya kwakuwa anafanya kwa maslahi ya Taifa.

“Rais Magufuli ameanza vizuri kwa kubana baadhi ya mambo ambayo hayakuwa ya msingi, kuna mambo mazuri sana mengi ameyafanya mapaka dakika hii, lakini mwalimu Nyerere alishawahi kusema kuwa wakati unafagia ni lazima uwe makini kwani unaweza kufagia hata shilingi, na sasa Rais Magufuli anafagia shilingi nyingi, kwasasa tumuache afanye kazi yake lakini tutamhukumu muda ukifika,”amesema Lowassa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here