SHARE

Beki wa pembeni wa Arsenal Hector Bellerin huenda akaihama klabu hiyo na kurejea mjini Barcelona Hispania kujiunga na FC Barcelona katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Bellerin ameonyesha kuwa tayari kuondoka kaskazini mwa jijini London, kufuatia kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na gazeti la Mundo Deportivo jana jumanne.

Beki huyo alisema suala la kuondoka ama kutoondoka Arsenal linategemea na wakati, kwa sababu hajui nini kitatokea kesho, kutokana na ufahamu alionao katika medani ya soka.

Alisema suala la usajili lipo wazi siku zote na inapotokea pande mbili zinakubaliana hakuna budi kwa muhusiaka kuondoka kwa sababu kitakachofanyika ni biashara.

“Nipo hapa kwa ajili ya kuitumikia Arsenal, ninaipenda na kuithamini, lakini likitokea la kutokea nitaondoka na kwenda popote pale ninapohitajika.” Alisema beki huyo mwenye umri wa miaka 22.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here