SHARE

Msanii na muandishi kutoka nchini Nigeria Wizkid Ayo amezidi kuongeza mashabiki kwa kolabo nyingine kubwa baada ya ‘Come Closer’ aliyomshirikisha Drake kwa sasa bado anazidi kuonesha kuwa focus yake zaidi iko nje ya Afrika.

Staa Wizkid akisubiriwa kwa hamu katika ziara yake ya shows nchini Uingereza ameachia audio ya kazi yake aliyomshirikisha staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown inayokwenda kwa jina #African Bad Gyal ambapo Chris kasikika akiimba katika miondoko ya kiafrika.

Hata hivyo moja ya kitu ambacho kilizua maneno na maoni tofauti katika kolabo yake iliyopita kwa Wizkid ni Drake kutoonekana katika video ya ‘Come Closer’ jambo ambalo linaweza kuzua hisia tofauti kama pia Chris Brown hatatokea katika video ya ‘African Bad Gyal’.

Vile vile kazi hii mpya kutoka kwa Wizkid iko katika orodha ya ngoma kali zitakazokuwa katika album yake mpya inayotegemewa kuwa na wakali wengine kama Trey Songz, Ty Dolla Sign, Diplo kutoka katika kundi Major Lazer na wakali wengine kibao kwa kuwa graph ya Wizkid kwa sasa inazidi kupanda kiasi cha kuamini anaweza kufanya staa yeyote wa muziki ambaye anaweza kuleta maana katika muziki wake.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here