SHARE

Gari lenye mwendo wa kasi zaidi duniani litakimbia kwa mara ya kwanza kabisa tarehe 26 mwezi Oktoba,

Gari litakimbia kwa kasi ya chini wakati wa majiribio kwenye uwanja wa ndege wa Newquay huko Conawall

Wahandisi wanataka kukagua mitambo yote ya gari hilo kabla ya kulipeleka nchini Afrika Kusini mwaka ujao, kukimbia kuvunja rekodi ya mbio ya kasi zaidi ardhini.

Kwa sasa rekodi ya kasi ardhini ni 763mph au 1,228km/h, na gai hilo linalofahamika kama Bloodhound litaongeza kasi kwanza hadi 800mph na kisha 1000mph.

Majaribio ya Newquay hayatafikia kasi kama hiyo kwa kuwa barabara ya mita 2,744 ni fupi kiliwezesha Bloodhound kushika kasi.
Badala yake dereva Andy Greren, ataliendesha gari hilo kwa kasi ya 200mph likitumia injini ya ndege aina ya Eurofighter-Typhoon

Itakua siku ngumu kwa Dereva Andy Green kwa sababu itakuwa mara yake ya kwanza kuliendesha gari hilo.

Matarajio ni kuwa Bloodhound litapelekwa eneo la Hakskeen Pan huko Northen Cape nchini Afrika Kusini kwa muda wa mwaka mmoja hivi unaokuja kajaribu kutimiza lengo lake,

Ili hilo liweze kufanyika, awamu nyingine ya uundaji wa roketi hiyo ni lazima ukamilike.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here