SHARE

Mdukuzi mmoja amefungwa jela baada ya kuiba karibu pauni 100,000 akitumia mfumo wa mtandao wa benki.

James Ejankowski, 24 aliibia benki ya Clydesdale and Yorkshire Banking Group zaidi ya pauni 99,000 mwezi Disemba mwaka 2016.

Kisha akatumia pesa hizo kununua magari aina ya BMW na Range Rover na pia akajichora chale usoni.

Alidanganya familia yake kuwa alikuwa ameshinda pesa hizo katika mchezo wa bahati nasibu.

Ejankowski aligundua kuwa ikiwa angetumia mfumo wa mtandao wa benki hiyo kuhamisha pesa kati ya akaunti zake usiku wa manane na saa saba asubuhi benki haingegundua.

Alitumia akaunti ya mpenzi wake Charlotte Slater kuhamisha pauni 53,399.

Licha ya kujinunulia vitu kadhaa Ejankowski, pia alitumia pesa zingine kulipa madeni yake na kampa shangazi yake puani 2000 na pauni 1,362 kwa baba mkwe.

Wiki nne baada ya kuanza kuiba, alijisalimisha kwa polisi na kukiri kuiba akisema kuwa alikuwa amebaki na pauni 40 tu.

Benki ya Clydesdale hata hivyo imefanikiwa kupata pauni 34,000.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here