SHARE
Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) ,akiwa amepiga picha ya pozi na mmoja wa wauza Karanga ambaye ameamua kuuza Karanga za Mwanamuziki huyo na kuachana na Karanga za Kawaida

Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akiwasili katika viwanja vya soko la Mchikichini
Meneja wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz), Salaam SK akizungumza katika Tamasha hilo.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) ,akiwa amepiga picha ya pozi na mmoja wa wauza Karanga ambaye ameamua kuuza Karanga za Mwanamuziki huyo na kuachana na Karanga za Kawaida.
Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akitoa Burudani kwa mashabiki wake waliofika katika uzinduzi wa Karanga zake uliofanyika katika Viwanja vya soko la Mchikichini Karume Ilala Jijini Dar es Salaam
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akizungumza na wakazi wa Ilala Mchikichini wakati alipokuwa akifanya shoo ya uzinduzi wa Karanga zake zinazokwenda kwa jina la Diamond Karanga zitakazouzwa madukani kote katika mfumo wa kisasa.
Mama mzazi wa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akiwa anakula Karanga za mtoto wake mara baada ya kuzinduliwa Karume jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) katika picha ya pamoja na wadau wake walionunu Karanga
Mashabiki wa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) wakigawana Karanga mara baada ya kuzinunua mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam
Mashabiki wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz).

=========

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Nchini Diamond Platnumz amewataka vijana kutochagua kazi za kufanya ili kupata kipato cha halali.

Diamond Ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa bidhaa yake mpya ya Karanga ‘Diamond Karanga’ ambapo amesema changamoto kubwa inayowakabili vijana kwasasa ni kuchagua kazi na matokeo yake huishia vijiweni na kuilaumu Serikali.

“Kabla ya Kuitwa Diamond mimi nimefanya kazi kadhaa ikiwemo kuuza mitumba na kupaka rangi nyumba, na kushona cherehani lakini yote hayo ilimradi tuu motto wa kiume nijipatie ridhiki yangu ya halali na ndio maana hata leo hii bidhaa hii imelenga watanzania wa hali zote”. Alisema Diamond

Aidha amesema kuwa bidhaa hiyo imetengezwa nchini na lengo ni kuongeza ajira kwa vijana na watanzania wote kwani kazi zote zinafanywa na wazawa na pia kuongeza thamani ya zao hilo kwa wafanyabiashara wadogo kutokana na upakiwaji wake.

 

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here