SHARE

Timu ya AFC Bournemouth inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England leo imeiongezea makali safu yake ya ushambuliaji baada ya jioni hii kumsajili bure mshambuliaji mkongwe, Jermain Defoe kutoka klabu iliyoshuka daraja ya Sunderland.
Defoe mwenye umri wa miaka 34 amejiunga na AFC Bournemouth kwa mkataba wa miaka mitatu utakaofanya awe akilipwa mshahara £65,000 kwa wiki na hivyo kuwa mchezaji anayelipwa vizuri zaidi klabuni hapo.
Defoe anarejea AFC Bournemouth kwa mara ya pili baada ya mara ya kwanza kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo msimu wa 2000/01 akitokea Ham United United na kufanikiwa kufunga mabao 18.
Akifanya mahojiano baada ya kukamilika kwa usajili wake,Defoe aliyefunga mabao 15 msimu uliopita amesema amefurahi kurejea kwa mara nyingine AFC Bournemouth na kuwataka mashabiki wa klabu watulie tuli awafungie mabao kama ilivyo kawaida yake.
Defoe anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na AFC Bournemouth katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya baada ya Asmir Begovic aliyetokea Chelsea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here