SHARE

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Christopher Chiza amesema  bodi hiyo ina mpango wa kuufanyia marekebisho Uwanja wa Sabasaba  kwa kujenga mabanda makubwa yenye hadhi ya kimataifa na hoteli kubwa ya kisasa.

Chiza ameyasema hayo leo wakati Rais John Magufuli alipokuwa akizindua maonyesho ya 41 ya kimataifa ya Sabasaba.

Chiza amesema  hoteli hizo zitajengwa ili baadhi ya washiriki kutoka nje na ndani ya nchi wazitumie  wanapohitaji wakati wa maonyesho hayo.

“Suala hilo lipo katika hatua za awali, utekelezaji wake unahitaji uungwaji mkono wa Serikali tunaomba utuunge mkono ili tuanze utekelezaji wa suala hili,” amesema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here