SHARE

Watu wanaodhaniwa kuwa magaidi wa kundi la la Shabab wamewachinja kwa kuwakata vichwa watu 9 katika shambulizi lililofanyika usiku wa kuamkia jana katika kijiji kimoja cha Kaunti ya Lamu huko pwani mwa Kenya.

Mauaji hayo yamefanyika siku kadhaa baada ya wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi kuua polisi watatu katika kijiji jirani cha Pandanguo.

Polisi ya Kenya imesema kuwa, wanaume wanane wameuawa kwa kukatwa vichwa katika shambulizi hilo.

Watu walioshuhudia wamesema, wanamgambo hao wamevamia vijiji vya Jima na Poromoko na kuuawa wanaume 9 na kwamba waliwachinja kama kuku kwa kutumia visu.

Wahanga wa mashambulizi ya al Shabab, Kenya

Wakazi wa vijiji hivyo wanasema, watu waliokuwa wamejizatiti kwa silaha wengi wao wakiwa na asili ya Somalia, walishambulia vijiji vya Jima na Poromoko usiku wa kuamkia leo wakisaka nyumba kwa nyumba na kwamba walikusanya wanaume 9 na kuwakata vichwa.

Mapema Ijumaa wakazi wa maeneo hayo walikuwa tayari wamewasiliana na polisi wakiripoti kuwa watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa al Shabab walikuwa wameingia vijijini humo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here