SHARE

Khalil Nazari, mvumbuzi na mtafiti wa Kiirani amefanikiwa kushinda tuzo maalumu na medali ya fakhari ya mashindano makubwa ya uvumbuzi ya INPEX nchini Marekani.

Uvumbuzi wa Khalil Nazari umehusisha uhuishaji majani wa ‘HL’ badala ya utumiwaji mafuta ya Mulch kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa hewa mijini. Mashindano hayo yaliwahusisha wavumbuzi 800 kutoka nchi 40 za dunia ambapo kijana huyo wa Iran ameweza kupata tuzo na medali ya fakhari ya INPEX nchini Marekani mwaka huu wa 2017 na hivyo kuweza kupeperusha bendera ya Jamhuri ya Kiislamu.

Uchafuzi wa mazingira duniani

Mashindano ya wavumbuzi ya INPEX nchini Marekani, yanahesabika kuwa mashindano makubwa ya uvumbuzi duniani. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikishika nafasi mbalimbali za kielimu katika maonyesho na mashindano tofauti duniani katika miaka ya hivi karibuni na hivyo kuifanya ihesabike kuwa mfano wa kuigwa kati ya nchi zinazoinukia kielimu na kimaendeleo. Mafanikio hayo ya Iran yanapatikana huku taifa hili likiwa limewekewa vikwazo vya kila upande na madola ya Magharibi hususan Marekani kwa zaidi ya miaka 30 sasa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here