SHARE

Mama yangu mzazi pamoja na Yule mama walienda wote mpaka kwa wale waganga, kumbe Yule mchungaji wa kanisa alikuwa anawafatilia kwa nyuma bila mama kujua, mama alipo ingia ndani kwa wale waganga akiwa na Yule mama, akawambia waganga kwamba, “nimemleta rafiki yangu kwenu na yeye yupo tayari kumtoa mwanae sadaka ili apate pesa, maana maisha ni magumu sana kwa upande wake” waganga wakasema, “mama vedasto unaharibu, umetuua tayari, kwanini unamleta adui yetu hapa,” mama akasema, “huyu sio adui, msaidieni na yeye” ndipo Yule mama akasimama na kusema, “nyie ndiyo mnatuharibia watoto wetu, naomba mtoe watu wote mlio wafanya misukule humu ndani” wale waganga wakachanganya dawa zao kisha wakaanza kumpulizia na kumu mwagia Yule mama” mama yangu akasema, “rafiki wewe siumesema unataka utajiri, kwanini unaongea maneno mabaya kama hayo” wale waganga waliendelea kumu mwagia Yule mama madawa ya aina mbalimbali, huku Yule mama pia akiendelea kuomba huku akilitaja jina la mungu, lakini wale waganga walimshinda nguvu mda ule, sasa kipindi imani ya mungu na ya kishirikina vinashindana, sisi tulio fanywa misukule mule ndani tulianza kulia, maana chumba kilijaa joto yaani kama moto umewashwa mule ndani, kipindi Yule mama anazidiwa na wale waganga maana walimshambulia sana, mchungaji nae alikuwa anawasili mda huohuo.

Mchungaji alianza kuomba huku akikemea nguvu za giza kushindwa, wale waganga walianza kulia huku wakisema, “tunaungua, motooo, tunaungua mungu tusamee”, wakati huo mchungaji ameshika biblia huku akiendelea kuomba kwa imani zote, watu walijaa sana lile eneo, waganga wakatoka nje huku wakiomba msamaa, kwamba, “usiendelee kumleta mungu tutakufa” ila Yule mchungaji aliomba sana bila kuwaachia.

Wale waganga walijaribu kutumia kila dawa zao ikashindikana, wakasema, “mama vedasto umetuua, mama vedasto tunakufa” mchungaji alikemea sana nguvu zao mpaka wakaanguka chini na kuanza kujikunja kama nyoka anavyo jikunja, huku wakiongea maneno ya ajabu kwamba, “sisi ni watu wa kutoka mbali, tumeua sana, tumeharibu nyota za watu, lakini tulifundishwa uchawi, unatuchoma moto unavyo omba, mungu ni adui yetu” mchungaji akasema, “toeni mitunguri yote nje, toa dawa zote za kishirikina kabla sijaendelea kuomba”, walitoa dawa zao zote nje, mafuvu ya watu na viungo vya albino, ndipo mchungaji akawaomba watu wavimwagie mafuta ya taa kisha wavichome.

Kipindi vile vitu vinaungua, watu walishangaa sana kutuona sisi misukule tunatoka mule ndani, tumepakwa dawa nyingi usoni, tupo kama wachawi kabisa, watu wakakimbia, ndipo mchungaji akasema “msiwaogope hawa ni wema, na walikuwa wanafanyishwa kazi humo ndani” ndipo tukaanza kuombewa, askari wakafika yale maeneo, kipindi maombi yanaendelea nilishangaa sana jinsi nilivyo kuwa maana nilikuwa kama mchawi kabisa, wale misukule wenzangu walikuwa wamekatwa ndimi hivyo walikuwa hawawezi kuongea tena katika maisha yao, wale waganga walipigwa sana na wanakijiji kabla askari haawajafika mpaka wakapoteza maisha, mchungaji alipata umaarufu sana na akaanzisha kanisa lake kubwa maeneo yaleyale na watu walimuamini hivyo akapata waumini wengi sana. Kipindi bado tupo yale maeneo, mama alianza kulia akisema, “nisamee mwanangu, siwezi kurudia, sikujua kama nimefanya kosa ni tamaa tu za dunia, naomba unisamee mimi mama yako,” nilimwambia kwamba, “mama siwezi kukusamee, maana wewe ni mtu mbaya sana, ulinifanyia mabaya mengi lakini nilijitahidi sana kusahau kisha nikarudi nyumbani, kumbe ulikuwa unataka kuniua, mama gani una roho mbaya kiasi hichi, ebu angalia bila huyu mchungaji ningeponaje humo ndani, watazame hao vijana wamekatwa ndimi zao na hawawezi kuongea tena katika maisha yao, na mimi ningekatwa je, leo hii ningekuwaje sasa, mama sikupendi na siwezi tena kurudi nyumbani, usingekuwa umenizaa wewe ningekufanya kitu kibaya sana lakini ngoja nikuache tu,” mama alikuwa analia huku akisema, “vedasto mwanangu, tazama jamii nzima imeisha gundua kuwa mimi ni mshirikina, nitakimbilia wapi sasa na wewe ndiyo mtoto wangu wa pekee” nilimwambia kwamba, “kila siku umekuwa ukimsingizia baba yangu ni mbaya eti kakufukuza kwake, kumbe wewe ndiyo hufai kabisa, sahau kama ulisha wai kunizaa”.

Watu walianza kumchapa mama na fimbo, kila mtu akaanza kumuita mchawi, wengine walisema “tumuue tu, kama alimtoa mtoto wake sadaka, sisi  ata tuua kabisa” mchungaji alikataa akasema, msimuue mchapeni tu mpaka akome, mwili wa mama ulivimba sababu alichapwa na kila mtu alie jisikia kuchapa, walipo ona amezidiwa wakamuacha palepale akiwa hoi. Ndipo watu wenye roho mbaya wakaenda mpaka kwenye nyumba ya mama kisha wakaichoma yote moto, vitu vya thamani vili teketea na moto, kisha wakaanza kubonda gari zake na mawe, wengine waliiba vitu, mpaka mama akaishiwa kila kitu akabaki na kiwanja tu.

Mama alipo pata nguvu pale chini, akasimama na kuanza kutembea ili arudi kwake, ila alishangaa kuona moshi umejaa kwenye nyumba yake, nyumba imewaka yote, pesa zake zote na vitu vikateketea mulemule ndani, mama alilia sana, maana alikosa sehemu ya kulala, kwasababu kila alipo enda kuomba msaada wa kulala japo siku moja aliambiwa kwamba, “sisi hatuwezi kulala na mchawi humu ndani, mfate vedasto wako akusaidie” mda mwingine mama alipo hisi njaa, alijaribu kuomba msaada kwa watu wampe chochote kusudi aweke mdomoni lakini hakufanikiwa. Ndipo mama akapata wazo la kujiua kusudi aondoke duniani, kipindi amefunga kitenge chake juu ya mti maeneo ya jirani kabisa na alipo kuwa amejenga kusudi aweze kujinyonga watu walimuona wakaenda kumzuia kisha walimchapa sana kwa jambo alilotaka kufanya.

Mama aliamua kujikaza mpaka akapata pesa kidogo ya mtaji ndipo akanunua nyanya ili aanze kuuza sokoni, kusudi asiendelee kulala nje pale kwenye kiwanja chake maana nyumba ilichomwa kikabaki kiwanja tu, lakini mtaji wote ulikufa, maana kipindi yupo sokoni hakuna ata mmoja alie mchangia nyanya zake, watu walisema, “hatuwezi kununua nyanya zako maana wewe ni mchawi, na wazazi walizuia na kuwakanya sana watoto wao wasi thubutu kununua nyanya kwa mama yangu, hivyo nyanya zote zilioza na biashara ikafa.

Mama akashindwa cha kufanya ila akapata wazo la kwenda kwa marafiki zake alio kuwa akifanya nao biashara pamoja ili wampe japo msaada wa chakula, ila alishangaa sana maana kumbe na wao walikuwa washirikina hivyo watoto walivyo toka kama misukule mule ndani wao pia walifilisika vibaya sana.

Mama aliendelea kuangaika usiku na mchana, hajui atakulaje na atalalaje pia, baadhi ya vijana wavuta bangi walikuwa wakorofi sana maana walikuwa wanambaka mama yangu usiku sehemu aliyo kuwa akilala, na hakuna ata mmoja alie msaidia mama, maana alitengwa na jamii nzima kwamba ni mshirikina, lakini hao hao vibaka walimsaidia mama, maana walikuwa wanamwambia asokote bangi wao wavute kisha wanamlipa elfu mbili tu ili aweze kula chakula, siku moja mama alikuwa amekaa tu, kiupele kidogo kikajitokeza  na kiliendelea  kukua mpaka kikaleta uvimbe mkubwa sehemu zake za siri, hivyo ugonjwa wake wa zamani ukarudi upya na hakuwa na pesa ata kidogo ya kununua dawa, hivyo akaendelea kukaa na kidonda hivyo hivyo tu.

Sasa mimi baada ya matukio yote sikuwa na jinsi nikaamua kurudi kijijini kule nilipo kuwa naishi, ila niliumia sana maana sikumkuta mwanangu, na Yule jirani akanisimulia jinsi alivyo tengana na mwanangu hivyo nikapata simanzi sana moyoni mwangu, sikuwa na jinsi nikaamua kusahau kwasababu nilijaribu sana kumtafuta mwanangu lakini ikashindikana.

Baada ya miaka tisa, nikiwa bado sijawai kuonana na mwanangu, siku moja nilipata wazo kwamba, niende kwa mama wa miti shamba ili nimpelekee japo mkungu wa ndizi, maana nilikuwa nimepanda migomba na ikazaa sana matunda, hivyo nikabeba mkungu wa ndizi ili nimpe kama shukrani maana alinisaidia sana kipindi cha nyuma.

Wakati nimefika kwa Yule mama, nilimkuta anaumwa sana, kulikuwa na baadhi ya ndugu zake wamekuja kumuuguza, ndipo Yule bibi akasema, “kijana wangu nashukuru sana kwa zawadi yako, lakini mimi naumwa sana na siwezi kupona, nilijaribu sana kukusaidia utoke kwenye imaya ya kishetani lakini nilishindwa maana walikuwa na nguvu sana, lakini zawadi niliyo kupa ni moja tu, nilimtibu mtoto wako mpaka akapona, na nimeishi nae sana hapa, ila kwasasa nimemtuma akafate dawa, maana kuna baadhi ya dawa nimemfundisha, utanisamee sana kwasababu niliamua kumuita jina kama la marehemu mtoto wangu, alikuwa anaitwa Kisiri, hivyo mtoto wako anaitwa hivyohivyo”.

Nilitamani sana kumuona mwanangu, sasa wakati namuuliza Yule bibi kwamba “mtoto wangu atarudi kwenye mida ya saa ngapi” nilishangaa kuona kimya, ndipo nikawaita ndugu zake, walipo mchunguza vizuri wakakuta tayari ameisha fariki” tulilia sana pale, maana niliumia ata ndizi nilio ileta hakuweza kuila.

Wakati nipo namsubilia mwanangu nilishangaa kuona kijana mkubwa anakuja, sikujua kama ni yeye nilihisi huenda ni mtu tu amekuja kwenye msiba, ila nilishangaa watu wanaanza kulia huku wakimwambia, “kaka kisiri bibi amekufa” nilimkimbilia mwanangu na kumkumbatia ila na yeye pia alishangaa sana maana alikuwa amenisahau, ila nilimwambia kuwa mimi ni baba yako, akakumbuka marehemu bibi yake mlezi, alimuelezea kuhusu mimi.

Nilimchukua mwanangu kisha tukarudi nyumbani, alinisimulia maisha yote aliyo yapitia mpaka kusaidiwa na Yule bibi, nikamuelezea pia kila kitu nilicho pitia yaani siku hiyo tulichelewa sana kulala maana tuliongea sana.

Niliendelea na maswala yangu ya kilimo ili mimi na mwanangu tupate kuishi maisha mazuri, na mwanangu akaamua kwenda mjini kutafuta pia maisha maana kuna watu alikuwa anafahamiana nao huko, sasa kipindi Kisiri yupo katika miangaiko ya kutafuta kazi alikutana na mwanamke mkubwa zaidi yake ila hakua mzee sana kwake, na walipendana sana, Yule mama alikuwa na pesa hivyo akampangia  kisiri chumba na mda mwingine walikuwa wakilala wote mpaka asubuhi, siku zingine hawakutani maana Yule mama alikuwa anaishi kwao yaani kwa wazazi wake maana alikuwa bado hajaolewa, mapenzi yali kolea sana baina ya mwanangu na Yule mama, mpaka watu wakaanza kumcheka kisiri kuwa anatembea na mtu mzima, lakini kila nilipo wasiliana na kisiri hakuwai kunieleza kama kapata mpenzi huko mjini alipo kuwepo, na nilishangaa maana alikuwa ananitumia pesa nyingi sana, ndipo nikaanza kujenga msingi kupitia zile pesa bila kujua mwanangu anatunzwa na kulelewa na mwanamke huko mjini.

Kwasababu Yule mwanamke alimpenda sana kisiri akajisahau mpaka akapata ujauzito wake, na kila walipo panga kuitoa ile mimba, Yule mama alikataa katakata maana alikuwa anaogopa sana kutoa mimba.

Maisha ya mama yangu mzazi yalikuwa magumu sana, maana ilifikia hatua ata wale vijana alio kuwa anawasokotea misokoto ya bangi, walimfukuza kwasababu kile kidonda kilikuwa kina toa harufu sana, na mama alikuwa aogi wala kujisafisha kutokana na ugumu wa maisha, ngozi ya mama ilifubaa sana, maana hakupata lishe nzuri na magonjwa pia yalikuwa yanamuandama, hivyo mama alikuwa ni mtu wa kujitenga, maana aliona aibu kukaa na watu, ila baadhi ya watu walikuwa wanamrushia makombo ya chakula na mama alikula tu kwasababu hakuwa na jinsi, wengine walimpa maji kusudi asife maana walijua akifa tu, basi jukumu litakuwa ni lao kuuzika mwili wake.

Sasa kutokana na mwanangu kumpa Yule mwanamke mimba, na Yule mwanamke alikuwa hataki kuitoa, hivyo akamwambia mwanangu kwamba, “mpenzi wangu, sahivi nina ujauzito wako, hivyo naomba unitambulishe kwenu mme wangu nikamuone baba yako ulie niambia yupo kijijini kusudi na yeye aje kwetu, ili wazazi wangu wajue nina ujauzito, nimechoka kujificha kila siku na natamani sana kuwa na mtoto” kisiri aliogopa kumleta mke wake maana alikuwa anamzidi umri, lakini alijikaza tu kwasababu Yule mama alikuwa anamsaidia mambo mengi sana.

Nilipigiwa simu na kisiri kuwa, “baba leo nakuja na mke wangu kumtambulisha, ili na wewe pia uende kwao kusudi tuweze kutambulika kifamilia” nilijindaa pia maana sikuwa na jinsi, kipindi wamefika kwangu nilichoka na niliishiwa nguvu hapohapo, kumbe mwanangu alikuwa amempa mimba mama yake mzazi bila kujua, maana alikuwa ni Queen nilie potezana nae miaka mingi tangu apelekwe Marekani, na huyuhuyu Queen ndiye alie mzaa kisiri alafu leo hii, amejikuta anaingia katika mausiano ya kimwili na mtoto wake alie mzaa, nilisema “queen mpenzi wangu, unatembea na mwanao”, akasema “nilikuwa sijui, mimi nilikutana nae mjini tu” kisiri akasema, “baba kwani huyu ndiyo mama yangu mzazi” USIKOSE SEHEMU YA 14


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here