SHARE

Konda wa daladala inayofanya safari zake kwa uelekeo wa Bububu-Uwanja wa Ndege, ambaye jina lake halikuweza kujulikana mpaka sasa amevamiwa na vijana wasio julikana huko visiwani Zanzibar na kumjeruhi kwa mapanga jambo lilipelekea kufariki kwake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanadai kuwa konda huyo alimpakiza kijana ambaye walianza kuzozana nae kwa kile kinachodaiwa kumpa pesa ambayo hailingani na eneo ambalo alishukia kijana huyo.

Inaelezwa kuwa kijana huyo alikuja na wenzake wapatao watatu na kumvamia na kuanza kumshambulia konda huyo kwa kumpiga na mapanga katika sehemu za mwili wake na kupelekea kuvuja kwa damu nyingi mwilini mwake.

Inaelezwa kuwa baadhi ya mashuhuda walishindwa kumsaidia kondakta huyo kutokana na vitisho vya vijana hao, huku ikielezwa kuwa hata dereva wa gari la kondakta huyo nae alikimbia baada ya uvamizi huo.

Tovuti hii ipo katika jitihada za kumtafuta Kamanda Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Hassan Nassir Ally kwa maelezo zaidi na uthibitisho wa tukio hili endelea kuwa nasi.

NB: Tunaomba radhi kwa matumizi ya picha hizi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here