SHARE

Siku Chache baada ya mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), Kutangazia umma kuwa amerejesha TRA fedha za mgao wa tegeta escrow alizopata Tsh. 40.4 milioni na kupewa risiti, TRA wameibuka na kusema hawazitambui fedha hizo.

Mkurugenzi wa elimu kwa Umma Wa TRA, Richard Kayombo amesema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi stahiki na siyo urejeshwaji wa fedha za kashfa kama Escrow.

“Fedha za escrow zinaihusu vipi TRA? Tunawezaje kukaa na kuzungumzia fedha ambazo si zetu? Mimi nashauri watafutwe wenyewe wazungumze kama wanataka kurejesha lakini siyo sisi” – alisema Kayombo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here