SHARE

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Nairobi mji mkuu wa Kenya umeuwa watu wanne hadi sasa tangu mwezi Mei huku serikali ikiifunga hoteli moja ya nyota tatu kwa jina la Jacaranda na mgahawa wa San Valencia mjini humo ili kudhibiti kuenea ugonjwa huo.

Imebainika kuwa watu kadhaa walihudumiwa chakula katika hoteli na mgahawa huo na baadaye walifikishwa hospitali baada ya kubainika kuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu.

Cleopa Mailu Waziri wa Afya wa Kenya amewaambia waandishi wa habari kuwa watu 79 wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta na wengine 12 katika vituo kadhaa vya afya jijini Nairobi na kwamba maafisa husika wanaandaa vituo kumi vingine vya kutolea matibabu kwa waathirika ili kudhibiti mlipuko huo wa waba.

Hospitali ya Taifa ya Kenyatta jijini Nairobi imepokea makumi ya watu walioonyesha dalili za kipindupindu  

Waziri wa Afya wa Kenya ameongeza kuwa hadi kufikia sasa wameshazifunga hoteli mbili na kwamba wataendelea kufanya hivyo iwapo itathibitika kuwa kuna hatari kwa umma. Serikali ya Kenya imeagiza kuchukuliwa vipimo haraka watu wasiopungua laki tano wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji vyakula katika muda wa siku 21 zijazo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here