SHARE

Maisha yaliendelea kuwa ya shida sana kwa upande wangu mpaka nikatamani kujiua niondoke tu duniani, maana sikuwa na uwezo wa kutoka nje ya nyumba ya Yule baba, na kibaya zaidi alikuwa anautumia mwili wangu vibaya sana. Nilivumilia kila kitu maana sikuwa na chochote cha kujitetea, lakini kilicho nikwaza na kuniumiza moyo kila baada ya sekunde ilivyo kuwa ikienda mbele, ni kwamba, “je Irene yuko wapi na anaishi vipi”, maana nilipotezana naye kituo cha basi na nilikuwa najua fika kuwa Irene hana ndugu yoyote mkoani kagera.

Siku moja nikiwa jikoni nampikia Yule baba chakula pamoja na vijana wake, nilisikia milio ya risasi sebreni, niliogopa sana kisha nikajifungia kwa ndani kusudi nisiweze kukamatwa na watu walio kuwa wametuvamia, baada ya mda nikasikia mlango kama umefungwa, kumbe tulikuwa tumevamiwa na majambazi, sasa kumbe wale majambazi walipo ingia walitaka kupewa pesa, lakini Yule baba aliwanyima pesa walizo kuwa wanataka, ndipo yeye pamoja na vijana wake wote wakapigwa risasi za kichwani kisha wakapoteza maisha mda huohuo.

Nilipo toka jikoni na kukuta wote wamefariki dunia niliogopa sana, kisha nikasema, “kila jambo lina maana yake duniani, maana Yule baba alinifanya mimi kama mke wake wa kumpikia chakula, lakini kumbe nisingekuwa jikoni na mimi pia ningekufa kwa kupigwa risasi kama wao” hivyo mimi kuwa mpishi wao, ndiyo ilikuwa ponapona yangu kufa.

Kipindi nipo sebreni nimezubaa, nilisikia geti linasukumwa, kumbe polisi walikuwa wanakuja pale ili kuangalia nini kinaendelea maana risasi zilisikika sana kutokea kwenye ile nyumba, hivyo wakajua kuna matatizo ndani, nilipo waona nikakimbia chumbani kisha nikaingia mpaka chooni ili wasinione maana nilijua fika kuwa lazima nikamatwe na kupelekwa kituo cha polisi ili nitoe ushahidi.

Polisi walitoa nje mili ya marehemu kisha wakaiweka kwenye gari lao na kuondoka nayo, ndipo nikatoka nje haraka kisha nikakimbia mida hiyo hiyo ya usiku bila kujua wapi naenda, ilikuwa ni usiku sana na kulikuwa na giza mno hivyo nilishikwa na uoga sana, maana hata nilipo utazama mti au matawi kwa mbele nilihisi kama ni watu wananifata mimi kumbe ni mimea tu inatingishwa na upepo.

Kulipo kucha nikaanza kuangaika kutafuta kazi ili niweze kupata chochote cha kuweka mdomoni maana nilikuwa na njaa sana, sikuweza kupata kazi siku hiyo na tumbo lilikuwa kama linaniuma kwa upande, kibaya zaidi hata midomo yangu ilikuwa imepata vidonda kidogo maana nilikuwa na njaa sana.

Maisha ya kisiri pia yalikuwa ya tabu sana,maana alikosa kazi pia hivyo akawa ni mtu wa kuangaika mda wote, siku moja alikutana na mama yake, kisiri akasema “mama za siku, shikamoo” queen akajibu, “za siku safi, ila tabia yako mbaya sana, nilikupa nyumba ukaikimbia, mali zote uka muachia bibi yako makusudi tu, ona sasa ulivyo chafuka mwili, unaonyesha kabisa hauna ata 50 mfukoni mwako” kisiri alimjibu kwamba, “bibi yangu ni mchawi sana, aliniwekea dawa za kichawi ndani ili mimi nimuachie mali zote,” kipindi kisiri anaongea na mama yake, queen alipigiwa simu na baba yake maana alitakiwa kusimamia baadhi ya kazi hivyo akaamua kuondoka na kuamuacha kisiri akiwa ameshika kichwa ila mama yake akasema, “kisiri mwanangu, nikiwa na muda nitakutafuta tuangalie biashara nyingine ya kufanya”.

Niliendelea kupata shida za hapa na pale, leo nakula kesho siri, lakini nilijikaza na nilikuwa najua siku ikifika nitapata kazi nzuri tu na mimi niwe tajiri.

Baada ya miezi kadhaa, mimba ya Irene ilikuwa kubwa, hivyo akaamua kutoka pale kituo cha basi maana kuna vijana watumiaji wa bangi, walikuwa wanamlazimisha Irene kufanya ngono akiwa na tumbo lake kubwa hivyo hivyo bila kujua sio jambo jema wanalo mfanyia.

Irene aliamua kuhama kutoka kwenye kituo cha basi kisha akaenda pembezoni na maeneo ya sokoni ili akae mwenyewe maana alikuwa anaogopa kukaa tena na wanaume. Tatizo ni kwamba, Irene alikuwa mjamzito na sehemu aliyo kuwa anakaa usiku hakuna mtu hata mmoja alie kuwa anakaa pale na kwa bahati mbaya zaidi uchungu wa mimba ulimshika bila hata mtu mmoja kuwepo, Irene aliogopa maana ndiyo ilikuwa mimba yake ya kwanza, alihisi kama atakufa lakini alijikaza na kusukuma mtoto, mungu alimsaidia akajifungua salama bila matatizo yoyote.

Maisha ya Irene yalizidi kuwa magumu, alijitahidi kupambana sana kumlea mtoto akashindwa, baada ya siku tano tangu Irene ajifungue mtoto, alijikuta anakosa pesa kabisa, ndipo akapata wazo la kumtupa mtoto ili aangaike yeye kama yeye kisha habari za mtoto aachane nazo,kweli Irene aliamua kuvuka barabara na kwenda kumlaza mtoto juu ya mbao alafu akamuacha analia huku mvua ikimnyeshea mtoto kisha yeye akakimbia na kwenda kujikinga sehemu aliyo kuwa akilala siku zote, mtoto alibaki mwenyewe, alilia sana maana alikuwa mchanga bado, Irene alipo fika sehemu alipo kuwa anakaa huruma ili mshika ya mwanae hivyo akaamua kurudi kuja umchukua mtoto wake, kipindi Irene anarudi na mimi pia nilikuwa napita hayo maeneo kutafuta banda lolote ili nijilaze mpaka asubuhi, ila kipindi napita nikasikia sauti ya mtoto, nilipo enda kumuangalia nikakuta kweli ni mtoto, nilihisi huenda ni mambo ya kishirikina nikataka kumuacha mtoto ila hisia za huruma zilinishika nikaamua kumbeba mtoto na kuondoka naye, ingawa nilikuwa na maisha magumu sana na nilijua nitateseka sana na mtoto kwa mda nitakae kua naye.

Sasa kipindi nimembeba mtoto na kuondoka kumbe mda huo huo, Irene pia alikuwa anafika ila kwa bahati mbaya hatukuweza kuonana.

Irene aliumia sana kukuta mtoto wake hayupo, akahisi huenda mbwa amemla mtoto wake, hakuwa na lolote la kufanya akaamua kuachana naye kisha akarudi sehemu yake ya kulala.

Nilimlea mtoto kwa tabu sana, niliangaika naye usiku na mchana, maisha yalienda hivyo hivyo mpaka mtoto akakua, niliamua kumuita mtoto wa Irene jina la kisiri, maana nilikuwa nampenda mtoto wangu pia hivyo nikaona nimpe huyu mtoto hilo jina maana alikua wa kiume hivyo nilikuwa nafarijika sana kumuita hilo jina, nilikaa miaka mingi sana kagera mpaka mtoto akafikisha miaka 13 nikiwa sijapata maisha na sijaonana bado na Irene.

Mtoto wa Irene alikuwa anapenda sana kuruka sarakasi, alikuwa anashangaza watu wengi sana maana alikuwa mtoto mdogo lakini akiruka anaweza kupaa juu na kujigeuza ata mara mbili hewani kisha anatua chini bila kushika wala kuanguka chini. Niliamua kutumia hiyo kama fursa ya kupata hela, maana nilianza kumwambia mtoto wa Irene kwamba,  “sahivi ukiruka kidogo unawambia watazamaji warushe mia mbili au chochote walicho nacho kisha unaruka,” kweli kisiri mdogo, alifanya hivyo na mungu alisaidia sana, maana hatukuwai kulala njaa tangu siku hiyo.

Siku moja kipindi mtoto wa Irene anaruka sarakasi zake kuna wazungu walimuona kisha wakaenda kumtazama, wale wazungu wawili walivutiwa sana na kipaji cha kisiri, ndipo wakamuita na kuongea naye kwa Kiswahili maana walikuwa wanakijua, wazungu walisema kwamba, “sisi tupo tayari kukupeleka Marekani ili ukakuze kipaji chako maana umebarikiwa na mungu hivyo unapaswa kupata mazoezi mazuri na baada ya mda utakuwa unalipwa pesa nzuri sana na utakuwa tajiri sana” kisiri aliwaleta wale wazungu mpaka sehemu tulipo kuwa tunalala, wale wazungu walishangaa sana kuona sisi tunalala kwenye kibanda” wakasema. “ukituruhusu kumpeleka mtoto marekani, na sisi tutakupa nyumba, gari pamoja na pesa zingine kwa biashara zako, lakini mtoto wako akianza kuingiza hela tutapunguza pesa zetu kidogo kidogo tulizo kuachia” sikuwa na maamuzi mengine nikakubali kisha wakaondoka naye.

Nilifatwa na gari lenye muonekano mzuri sana kisha nikapelekwa kwenye nyumba yangu niliyo pewa na wale wazungu alafu nikaachiwa pesa, tangu kipindi hicho nilisema siwezi kufa tena masikini, mtoto wa Irene alipanda ndege na kuondoka kwenda marekani.

Nilianza kufanya biashara mungu saidia watu waliniamini na kila mfanya biashara pale alikuwa na namba yangu kwa ajili ya kuagiza mizigo, biashara zangu zilikuwa ni kila siku mpaka nikanunua gari ya kununulia mizigo ya biashara, mungu alisaidia sana nikaanza kujenga nyumba mpya, jina langu lilikuwa kubwa sana ndipo nikaanza kuajili watu mbali mbali kwa ajili ya kusambaza bidhaa kila kona.

Irene alikuwa anasikia jina langu linakuwa kubwa sana kila sehemu  wanasema, “vedasto ni mtu mzuri sana, hana tamaa, anafaa sana” lakini Irene hakutaka kumfatilia ni vedasto gani maana alijua fika kuwa vedasto anaye mjua hawezi  kuwa tajiri.

Kwa kipindi kile cha nyuma nilipo kuwa nimetekwa sikuwa tena na mawasiliano ya simu maana nilinyang`anywa mawasiliano yangu nisiweze kuwasiliana kipindi chote nilipo kuwa nimetekwa hari ya kisiri nilikuwa sijui kabisa anaendeleaje.

Kutokana na maisha ya kisiri kuwa magumu aliamua kuanza kutafuta kazi yoyote afanye maana alizidiwa kiasi cha kwamba angezubaa kidogo tu basi angekufa kwa njaa.

Kutokana na mama yangu mzazi kuhudumiwa vizuri na baba queen, kila siku baba queen alikuwa anamsifia mama yangu kwamba, “tangu nimekusaidia wewe kukaa hapa, biashara zangu zinaenda vizuri mama yangu” ndipo mama akamwambia baba queen kwamba, “mungu atakupa zaidi baba, lakini baba yangu naomba unitafutie kijana aweze kunisaidia kazi za hapa maana naangaika” baba queen akasema “sawa usijali kesho nakuletea kijana wa kazi”.

Baba queen alimtuma kijana wake ili amsaidie kutafuta kijana wa kazi ili huyo kijana amsaidie mama yangu mzazi kazi za ndani, sasa sikumoja kisiri amekaa mtaani njaa inamuua, alikuja kijana kisha akasema, “samahani nilikuwa natafuta kijana wa kazi za ndani” kisiri alikuwa hapendi hiyo kazi lakini aliikubali tu maana maisha yalikuwa magumu sana kwa upande wake na alitamani kupata sehemu ambayo uhakika wa kula upo. Yule kijana alimpeleka kisiri mpaka kwa mama yangu mzazi kusudi aweze kufanya kazi, kumbe siku hiyo baba queen alikuwemo ndani maana alikuja kumsalimia mama yangu.

Sasa kipindi kisiri ameingia ndani na kumkuta baba queen pamoja na mama yangu akasema, “bibi umefata nini huku,” kisiri akaambiwa huyu ndiyo utakae mfanyia kazi, kisiri alikataa akasema, “huyu ni bibi yangu siwezi kumfanyia kazi namchukia sana ni mchawi hata niua” baba queen akasema, “ ehhh kumbe nimemsaidia mama vedasto, heeee jamani sikujua wewe mama naomba uondoke kutoka nje sikutaki humu” mama yangu alilia sana lakini baba queen akasema, “nauchukia sana ukoo wenu wote, na ningejua kuwa wewe ni mama vedasto nisinge kusogelea ata kidogo, nisinge kupa ata salamu, naumia sana umekula mali zangu kwa mda mrefu, naomba utoke kwenye hii nyumba haraka”, mama yangu alianza kuwaza tena habari za kulala nje, akasema “wewe kisiri umefata nini huku, ona sasa umeniharibia maisha mazuri”baba queen akasema, “wewe mama unachelewa toka haraka nje ya nyumba sikutaki kwangu maana wewe ni mshirikina”. Ndipo mama akatoka nje na kuendelea kulala nje na kupata mateso yake ya siku zote, kisiri alikosa ile kazi lakini hakuumia ata kidogo maana alikuwa hampendi bibi yake hata kidogo.

Siku moja usiku nilikuwa ndani nimelala sana, maana nilikuwa na usingizi mwingi kiasi kwamba sikutaka kusumbuliwa ata kidogo, mara ghafla damu zikaanza kutoka mdomoni na puani alafu nikapata ndoto ya ajabu sana isemayo kwamba,

(Usikose sehemu ya 24)


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here