SHARE

MGANGA wa jadi, Levocatus Kanjalanga (65), ameuawa kwa kuchomwa na mkuki mgongoni na mtu ambaye anadaiwa kuwa ni mteja wake wa muda mrefu.

Ilielezwa na mashuhuda kuwa mtu huyo alikuwa akimlalamikia mganga huyo kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akimtibu kwa kumtoza fedha nyingi, lakini haponi maradhi yanayomsumbua.

Mtoto wa mganga huyo aliliambia gazeti la Nipashe kuwa baba yake aliuawa juzi saa 1:30 asubuhi kwa kupigwa mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani katika Kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani humo.

Alisema kwa muda mrefu watu ambao walikuwa wakitibiwa na baba yake walikuwa wakilalamika kutozwa fedha nyingi pamoja na mifugo, lakini hawaponi, hali iliyosababisha kuanza kumuona kama tapeli.

Alisema watu hao walikuwa wanalalamikia na kutofanikiwa matatizo yao ya kiafya, kutafuta mali pamoja na mazindiko.

“Pengine malalamiko hayo ndiyo yaliyosababisha mtuhumiwa aamue kumuua kwa kumchoma mkuki mgongoni, na aliyefanya tukio hilo hajapatikana na mkapa sasa anatafutwa,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anasakwa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here