SHARE

SEHEMU YA 17.

“Dahh! Yaani Meshack mwanangu unalala na mama yako, unanivua nguo Meshack”, “hapana baba, nisamee ni mama alinilazimisha kufanya hivi” nilimjibu hivyo huku mwili wangu wote ukiwa unatetemeka, sehemu zangu za siri zikiwa zimesinyaa yaani ilikuwa ni aibu tupu, maana nilijua fika kuwa siku ya mwizi imenifikia, “Meshack mwanangu, nimekulea kwa upendo wote, nimekusomesha kwa pesa zangu kwa tabu sana, haya ndiyo matunda ninayo vuna kwako, unakula ninapo kula, ehh laana gani hizi Meshack, nimemkosea Mungu nini mimi?” alisema baba huku machozi yakimtiririka, “nisamehe baba siwezi kurudia, ni shetani tu”. Mama alikuwa amezubaa akashindwa hata kuwamka ili avae nguo maana alikuwa bado uchi kama mimi, baba akasema, “nimeamini maombi yanasaidia sana, nilijikuta narudi nyumbani bila sababu maarumu, kumbe huu ushenzi ndiyo unatendeka ndani ya nyumba yangu, mmenivua nguo leo, yaani sikutegemea kama kijana wangu ungeweza kufanya jambo kama hili, kumbe ndiyo maana mchumba wako alikukimbia, yaani nakulazimisha kuoa kila siku hutaki kumbe unazini na mke wangu, hivi kumbe ndiyo maana mke wangu kipindi anajifungua alikuwa anakutaja sana jina, leo ndiyo nimejua kumbe hata mtoto sio wangu”, “hapana mume wangu mtoto ni wako” alisema Fey, baba alitoka chumbani kisha akaingia chumbani kwake kwa hasira, kipindi hicho sisi tupo chumbani, kisha baba akakaa ndani.

“Mama unaona ulicho fanya sasa, hivi naificha wapi sura yangu jamani, nimekuzuia kila siku hii tabia lakini umekuwa ukinilazimisha kila siku, tazama aibu iliyo tupata, nitaishi vipi sasa hapa nyumbani, ni bora nitoroke tu, siwezi kuvumilia hili swala hata kidogo” mama akasema, “usiondoke mpenzi wangu, baba yako siku hizi ni mtu wa kanisani sana, naamini atatusamehe, maana wanafundishwa kusamehe, kisha tutaendelea kujivinjari bila mtu yoyote kugundua, najua jinsi ya kumlaghai baba yako wewe subiri”.

Mama alitoka chumbani kwangu kisha akaenda kwa mume wake ili aombe msamaha maana alikuwa anajua udhaifu wa baba, baba alikataa kabisa kumsamehe, kipindi wanaendelea kugombezana, mtoto akaamka kisha akaanza kulia, sasa kwakuwa baba alikuwa  amezoea kumbeba mwanae kila aamkapo, hivyo mama akahisi hata siku hiyo itakuwa hivyohivyo, lakini cha kushangaza alimwambia mama kwamba, “mchukue mwanao kisha utoke kwangu”.

Mama alimchukuwa mtoto, ili aniletee chumbani, lakini cha kushangaza alipo ingia chumbani kwangu akakuta tayari nimeisha toroka. Niliamua kupanga chumba sehemu nyingine, ili nisionane na baba kwanza maana nilijua kuwa lazima amekasilika sana, kumbe baba alichukia sana akaenda sehemu niliyo kuwa nafanyia kazi kisha akawambia mambo niliyo yafanya, sasa kwakuwa bosi wa ofisini kwetu alikuwa anafahamiana na baba, wakaamua kuniachisha kazi, niliishiwa pesa huku kazi pia sina, ndipo nikaamua kutoroka na kwenda mkoa mwingine mbali kabisa na nyumbani kusudi nisiweze kuonana na baba.

Kumbe kipindi hicho chote mke wa baba alikuwa hana sehemu ya kuishi, maana kumbe hata ndugu na marafiki wa mke wa baba walikuwa wana taarifa kuwa yeye na mimi tumefumwa ugoni, hivyo ndugu zake pia wakamfukuza ndipo mke wa baba akakosa muelekeo wa maisha kabisa.

Nilikimbilia mkoa wa Mara, mpakani mwa Kenya na Tanzania (sirari) ili nisijulikane nipo wapi kabisa, pesa yangu iliisha nikabaki bila chochote mfukoni, ndipo nikajaribu kutafuta kazi kwenye offisi za uhamiaji kule kule mkoa wa Mara kusudi niweze kukidhi mahitaji yangu. Mungu alisaidia nikapata kazi maana walipenda vyeti vyangu kwasababu nilikuwa na matokeo mazuri ya shule.

Maisha yaliendelea, lakini nilikuwa nakosa raha mda wote, kila ninapo kaa nakumbuka tu dhambi niliyo ifanya nyumbani, nilijikuta naanza kunywa sana pombe, mshahara wangu wote unaishia kwenye (bar) kutokana na kunywa sana pombe ikanifanya nikawa nachelewa sana kazini, walijaribu kunionya sana ikashindikana, hata kuna mda mwingine nilikuwa nazubaa kila mda ofisini maana nilikuwa najikuta tu namuwaza baba yangu je ananifikiriaje?.

Nilipewa barua pia ya kufukuzwa kazi pale ofisini hapo ndipo nilichoka kabisa, maana nilijua fika kuwa maisha yangu yatakuwa ya tabu sana.

Siku moja nilimpigia rafiki yangu simu ili anipe habari za huko kwa baba yangu niweze kujua anaendeleaje, akasema, “dahh, Meshack umeharibu sana huku ndugu yangu, baba yako ameisha mfukuza mke wake pamoja na mtoto, maana anasema mtoto ni wako, na kibaya zaidi ni kwamba, mama yako pamoja na mtoto wanaangaika sana huku, leo utamkuta mama yako sehemu za pombe, kesho utamkuta anafanya kazi za kupasua kokoto na mtoto wake mgongoni, siku zingine anakuta amebakwa na vijana wa mtaani, huwezi kuwamini sahivi mama yako anavuta sigara hadharani, jitahidi urudi ukomboe familia ndugu yangu”. Nilipo sikia yale maneno palepale nikakata simu maana niliona kabisa kama baba na upole wake wote ule kamfukuza mama na mtoto, basi hawezi kunisamehe hata kidogo. Kwasababu kipindi nina kazi nilikuwa nakunywa sana pombe, hivyo hata nilipo kosa pesa wale walevi wenzangu nilio kuwa nikiwanunulia wakaanza kuninunulia pia, sasa kutokana na shida na ukosefu wa kazi ulio kuwa unanikabiri, mmoja wawale walevi wenzangu akaamua kunipa gari lake kusudi niwe nampelekea watoto wake shule kisha atakuwa ananilipa kila baada ya mwezi.

Siku moja nipo njiani napeleka watoto shule, kwa bahati mbaya niliona kama kuna gogo katikati ya barabara, hivyo nikalazimisha kukwepa lile gogo kumbe pembeni kulikuwa na baba yuko na familia yake wanatembea, kwa bahati mbaya nikamgonga na kumpasua mguu wake. Niliogopa kuwa naweza kukamatwa ndipo nikaachana na Yule baba akiwa analia nikawasha gari na kukimbia. Yule baba alishindwa kutibiwa ule mguu ndipo wakaamua kumkata hivyo basi nikawa chanzo cha kumfanya awe kilema, siku moja nilikutana naye barabarani akiwa anatembelea gongo, nikashikwa na moyo wa huruma ili nimuombe msamaha lakini nikaogopa kabisa kumfata. Kumbe ndugu wa Yule jamaa walichukia sana kwa kitendo nilicho mfanyia ndugu yao ndipo wakaanza kufanya mikakati ya kunifanya kitu kibaya ili walipize na wao kisasi.

Siku moja nipo (bar) nakunywa, pombe zikanikolea sana, kwa bahati mbaya nikamshika mke wa mtu makalio yake bila kujielewa maana mimi nilihisi huenda ni dada tu anaejiuza kutokana na mavazi yake aliyo kuwa amevaa. Mume wake alichukia kile kitendo cha kushika makalio ya mke wake. Ndipo akaongea na vijana wake wanikate mkono wangu kisha wampelekee. Mimi sikujua na wala sikuwa na taarifa yoyote kuwa kunamtu anahitaji mkono wangu.

Siku moja usiku nikiwa nimetoka kupeleka gari la bosi wangu kwake, nilishangaa kukutana na vijana wawili barabarani huku wakiwa wameshika panga, “tunataka mkono wako wa kushoto, tumetumwa na bosi, hatuna shida ya kukuua”, walisema hivyo, “ndugu zangu mkono wangu wa nini tena naombeni mnisamehe bwana, chukueni hela hii hapa misinikate mkono” wakachukuwa hela kisha wakasema, “tusipo peleka mkono wako tutakatwa sisi, turuhusu tu tukate mkono wako” niliinama chini kisha nikawakwepa na kukimbia, nilipo fika mbele kidogo nikakuta ukuta hivyo nisinge weza kukimbia tena, jamaa mmoja alinyanyua panga kisha akawa kama anataka kukata shingo langu ndipo nikakinga mkono  wangu wa kushoto kweli ukakatwa na kisha wakauchukuwa ule mkono mpaka wa bosi wao.

Niliangaika sana kuuguza kile kidonda, na nilijua tu kuwa haya matatizo yote ninayo yapata ni sababu ya laana ya baba yangu mzazi. Bosi wangu aliamua kuniachisha kazi maana hakutaka tena niwaendeshe watoto wake kwa kutumia mkono mmoja.

Siku moja nikiwa ndani nalia tu, huku nina mawazo chungu nzima, nikaanza kukumbuka jinsi baba alivyo kuwa ananipenda leo hii nateseka na dunia peke yangu yaani mda mwingine nakosa hata elfu moja mfukoni, wakati najifuta machozi nikasikia simu yangu inaita nilipo itazama kumbe baba yangu ndiyo alikuwa na shida ya kuongea na mimi.

SEHEMU YA18.

Nilipokea simu ya baba kwa furaha nikihisi huenda ana lengo la kunisamee, “hallo habari Juma, vipi pesa yangu unanipa lini” alisema baba, “hapana baba mimi sio Juma, ni mwanao Meshack”, alinisonya kwanza, “hivi kumbe nimekupigia wewe mpuuzi, na sitaki kusikia unasema wewe ni mwanangu, nilisha hesabu tangu zamani kuwa sijawai kuwa na mtoto, na ninaomba kama nikijisahau nikakupigia wewe tena usipokee simu yangu, tafadhali sana” alisema baba kisha akakata simu, nilichoka nikajua moja kwa moja kuwa sina msaada tena wa maisha, ndipo nikaamua kutoa (line) ya simu kisha nikaitupa ili nisipatikane tena kwenye simu baada ya hapo nikanunua line mpya hivyo mimi na baba tukapoteza mawasiliano ya kwenye simu tangu siku hiyo.

Sehemu nilipo kuwa nimepanga, kodi ilikuwa imekaribia kuisha na kibaya zaidi sikuwa na pesa kabisa, ndipo nikaanza kutafuta kazi kila nyumba, niliangaika sana maana kila mtu alikuwa ananiambia kuwa, “wewe huna mkono mmoja, utafanyaje kazi?” mda wote nilikuwa nalia mpaka napiga magoti chini kusudi nipate angalau kazi yoyote niweze kutunza pesa kwa hajiri ya kulipa kodi, nilizunguka sana lakini sikufanikiwa ndipo nikaamua kurudi nyumbani, kipindi nafika mlangoni kwangu nikakuta mlango wangu umebomolewa, nilipo ingia ndani sikukuta begi langu la nguo, kumbe wezi walikuwa wameniibia, kibaya zaidi vyeti vyangu vyote vya shule na kuzaliwa vilikuwa kwenye ilo begi, hivyo nisingeweza kuomba kazi bila vyeti tena kupitia helimu yangu, na kila nilipo pata wazo la kuvifatilia, gharama zake zilikuwa juu ya uwezo wangu, ndipo nikakata tamaa kabisa na maisha, lakini nilikuwa najua haya yote yanayo nitokea ni laana ya baba yangu mzazi.

Hali iliendelea kuwa ngumu mpaka kula kwangu kukawa kwa tabu sana, kilicho kuwa kina niumiza sana ni pale kazi zilizo kuwa zinapatikana zilikuwa za kulima kwenye mashamba lakini mimi nilikuwa siwezi kulima kutokana ule mkono mmoja kukatwa. Siku moja nilizidiwa sana maana nilihisi njaa mpaka nikaanza kuhisi mwili unaishiwa nguvu kabisa, ndipo nikamsimamisha dada mmoja hivi barabarani Mungu saidia alisimama, “habari dada, ndugu yangu naomba msaada wako, leo siku ya nne sijaweka chochote tumboni, naomba hela nikale dada”, “ehh kaka siku nne hujala, unaishi vipi sasa?” alijibu hivyo, “nishida tu za dunia dada yangu”, “sasa cha kufanya ni kitu kimoja kaka yangu, twende kwetu nikapike chakula ule maana hapa sijabaki na hela yoyote kabisa” niliongozana naye mpaka kwao, alipika chakula tukala pamoja na wazazi wake, familia yao ilikuwa imeshika dini sana, hivyo nikalialia sana shida zangu mpaka baba wa Yule binti Nancy, akanionea huruma, hata mama Nancy akasema, “wewe kijana usijali kabisa, utakaa hapa utaishi tu vizuri maana sio vizuri sisi kubakiza chakula kisha tunatupa wakati  wewe unasema unakaa siku nne hujala chochote”.

Nilianza kuishi kwenye ile nyumba, ila nilijitahidi sana kufanya kazi nilizo ziweza, mpaka wazazi wa nancy na Nancy wote wakafarijika mimi kuendelea kukaa kwao. Niliishi kwa mda sana kwenye nyumba yao, baada ya miaka saba, baba yake Nancy alifariki dunia hivyo nyumba nzima tukabaki mimi, mama Nancy pamoja na Nancy. Tuliishi vizuri sana pale nyumbani na walikuwa wananiheshimu sana maana ndiyo nilikuwa mwanaume nilie kuwa nimebaki kwenye ile nyumba. Siku moja tumekaa sebreni mama Nancy akaanza kututania kwamba, “hivi nyie wanangu si muoane tu mniletee wajukuu maana mnapendana sana, mda wote mnafurahi tu, nyie hamjui tu yaani mnapendeza sana kuwa mke na mume, na mimi natamani sana kuona wajukuu zangu kabla sijafa”.

Kwa mara ya kwanza nilihisi huenda mama anatania, hivyo basi nikaamua kumuita Nancy pembeni kusudi tuweze kuongea kuhusu ilo swala, sikuwamini nancy alivyo sema kwamba yupo tayari kuwa mke wangu, “Nancy asante sana kwa kunipenda na kunikubalia kutoka moyoni mimi kuwa mume wako, nashindwa kuwamini yaani na huu ulemavu wangu umekubali kuwa mke wangu wa maisha”, “mapenzi huwa yanatoka moyoni Meshack, napenda sana tabia zako tangu nikufahamu, maana kipindi chote upo hapa sijawai kukuona na tabia mbaya za kubadilisha wanawake”.

Mama Nancy alitukubalia hivyo nikaanza kulala chumba kimoja na nancy, nilifurahi sana maana alikuwa ananifariji sana, mda mwingine nikajisahau kabisa kama kuna kosa nililitenda kwa baba yangu. Baada ya miezi miwili Nancy alipata ujauzito, Mungu alisaidia mpaka akajifungua, lakini tulishangaa sana maana mtoto alitoka akiwa kilema yaani mguu mmoja mfupii mwingine mrefu, Nancy aliumia sana kupata mtoto wa namna ile ila nilimpa moyo kuwa yote ni mipango ya Mungu, baada miaka miwili mke wangu alipata ujauzito, nilikwazika sana maana mtoto alie toka tena alikuwa kilema kama wa kwanza, yaani mguu mmoja mrefu na mwingine mfupi, mke wangu akauliza, “Meshack mume wangu, hivi kwenye ukoo wenu kuna ndugu wa namna hii, mbona watoto wetu wote wanatoka vilema” nilimjibu kuwa, “mke wangu kwa upande wetu sijawai kuona kabisa ndugu zetu wapo hivi labda nikuulize kwenye ukoo wenu kama wapo wa hivi, maana watoto wetu wote wanatoka vilema tu” tulikosa jibu kabisa, ndipo tukapanga kuwa tutafute mtoto wa tatu kama na yeye atakuwa kilema basi tuache kuzaa tu, ili tuwalee watoto watatu tu, tuliumia sana maana hata mtoto wa tatu sawa alikuwa wa kike mrembo sana lakini nayeye alikuwa kilema pia.

Nilikaa nikawaza sana kwanini iwe vile, ndipo nikamuita mke wangu ili nimpe siri kwa nini tunapata watoto wa namna ile, alipo kuja nikamwambia kwamba, “mke wangu kuna kipindi nilikuwa dereva wa gari, ila kwa bahati mbaya nilimgonga mtu barabarani na kumpasua mguu wake, baada ya hapo nilimkimbia, hata sikuwa na punje ya huruma kuweza kumjulia hari hospitali kipindi anakatwa ule mguu, na kuna siku moja nilikutana naye barabarani anatumia gongo kutembea nikatamani sana kumuomba msamaha ila nikaogopa, mimi naomba twende kumuomba msamaha popote alipo kusudi tusiendelee kupata vizazi vya namna hii, huenda Mungu na yeye pia atanisamehe, endapo Yule baba akitusamehe kutoka moyoni, mke wangu akasema, “sawa mume wangu tumtafute, maana hii ni laana”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here