SHARE

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kuwa Tamasha la Usalama Barabarani ambalo lilitarajiwa kufanyika Agosti 5 mwaka huu litafanyika Agosti 12 mwaka huu Viwanja vya Taifa vya Uhuru Dar.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo,  Masauni amesema sababu za kuahirishwa kwa tamasha hilo inatokana na kuwepo kwa tukio la kihistoria la uzinduzi wa bomba la mafuta huko mkoani Tanga, uzinduzi unaofanywa na Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni na kuhudhuriwa na mawaziri wa pande zote mbili.

Ameeleza kuwa tamasha hilo linatarajia kuwakutanisha wasanii maarufu katika tasnia ya filamu (Bongo muvi)na muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva na bendi za muziki  wa dansi.

“Tamasha hili litapambwa na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukimbia pamoja ‘jogging’ kwa kushirikisha vikundi mbalimbali na timu ya wabunge

“Katika kutekeleza mpango mkakati wa awamu ya pili, tumejikita katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji mbalimbali wa barabara hususan kwa vijana ambao kwa mujibu wa takwimu zetu za ajali ni kundi linaloathirika zaidi kwa ajali za barabarani hususan  madereva wa pikipiki na hivyo malengo ya tamasha ni kuweza kufikiwa na kusaidia katika kupunguza ajali za barabara,”alisema.

Msanii Msaga Sumu akifurahia jambo na Mkurugenzi wa WCB Salam Ashirafu.

Wakati wa tamasha, mabalozi wa usalama barabarani watapewa tuzo, zawadi na vyeti vitatolewa kwa wadau wa usalama barabarani na wale waliochangia kufanikisha tamasha. Mgeni rasmi wa Tamasha hilo anatarajia kuwa Rais Magufuli.

PICHA ZA WADHAMINI 

Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bakhresa, BINSLUM, na  Benki NMB, ambapo NMB wamedhamini kiasi cha shilingi milioni 10, huku BINSLUM wakitoa jezi seti nne na kampuni ya Bakhresa kupitia chombo chake cha habari na bidhaa zake watarusha moja kwa moja Tamasha hilo.

Mwakilishi kutoka kampuni ya Bakhresa


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here