SHARE

Kuelekea ukingoni kabisa mwa dirisha la Usajili wa ligi kuu Tanzania bara Singida United imemsajili mshambulizi wa Kaizer Chiefs Michelle Katsavairo kwa mkopo ikiwa imefunga usajili wa wachezaji wa kigeni.

Singida United na Kaizer Chiefs zimekubaliana kuhusiana na Katsavairo mchezaji ambaye anaaminika ni mkali kwa kufunga hasa kwa mashuti makali.

Katsavairo sasa anaungana na wachezaji wengine wa safu ya ushambulizi ya Singida United kama Simbarashe Nhivi, Danny Usengimana, Atupele Green na Katsairo Michelle raia wa Zimbabwe aliyetua leo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here