SHARE

SEHEMU YA 1.

Ilikuwa ni siku ya jumapili tarehe 27/10/1994 mida ya usiku nikiwa mdogo bado. Baba alikuja nyumbani akiwa amelewa sana, tulishangaa maana alikuja na mwanamke anaejiuza! Alimuita mama akamwambia “mke wangu nimeleta mke wa pili, naomba umuheshimu ndani ya hii nyumba” Mama akajibu,haa! Mme wangu tabia gani hizi? Unaleta mwanamke bila kunihusisha unasema tu umeleta mke. Mama akasema,we binti naomba tu urudi kwenu mme wangu amelewa ndo maana kafanya maamuzi mabaya. Yule mwanamke akasema,”Haa! Naomba unikome hapa ndo nimefika sufuria moja mwiko mmoja”
Mama akamuuliza “nini? Yani nakuomba kistarabu unanijibu ovyo, Ngoja nikupe adabu yako.”
Ndipo mama akafunga kitenge kiunoni akitaka kumpiga. Binti nae alikuwa na nguvu wakaanza kuangushana na mama. Mimi nilikuwa mdogo nisingeweza kumsaidia mama.

Ila nilisikitika sana pale baba na yule mwanamke walipo anza kumchangia mama kumpiga. Hivyo basi mama hakuwa na jinsi ndipo akaamua kukubali. Lakini mama alihisi anaonewa maana mapenzi yalipungua sana kwake alipendwa sana mke mdogo. Mama alionekana mchafu lakini mke mdogo alipendeza sana, Mama alivumilia kwa kila jambo maana alikuwa anampenda baba.
Siku moja asubui baba alicharuka akamfukuza mama bila sababu. Baba Akasema na nikiwa nasikia kwa masikio yangu.
“We mwanamke ni kin’gan’ganizi kweli, nakuletea mwanamke ndani tena nawalaza wote kitanda kimoja! Bado huondoki tu!” Mama alianza kulia pale majirani walipo kuwa wanamcheka kinafiki. Mama akasema asante mme wangu kisha akanibeba nakusema mwanangu tuondoke
Baba akasema ondoka mwenyewe mwanangu muache. Mama simuachi mwanangu, huyo mkeo ana roho mbaya atanitesea mtoto.

Baba akanivuta mama nae akawa ananivuta kila mtu ananitaka maana nilikuwa mtoto mmoja tu! Nilivutwa mpaka nikaanza kulia kwa maumivu.
Mama yangu  iliondoka akiwa analia sana, maana mama alikuwa yatima na hakuwa na ndugu yoyote wa kumsaidia, msaada wake mkubwa alikuwa ni baba tu. Nililia mama  alivyo ondoka maana nilikuwa nampenda. Mama alikosa pa kulala.
Kipind mama yupo mtaaani bila msaada  alibakwa na vijana 7 usiku! na ndipo mimba ya mdogo wangu wa kike ikapatikana pia, doh  maisha ya mama yalizidi kuwa magumu.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here