SHARE

SEHEMU YA 2.

Maisha ya mama yalikuwa magumu lakini alijitahid kujishugulisha na kazi za kwenye migahawa ili apate kula yeye na mwanae.
Sehemu ya kulala bado ilikuwa ni shida hivyo mama akawa kama mlinzi wa mgahawa alipokuwa akifanya kazi maana alilala humohumo bila ata shuka au godoro tena sakafuni kwenye baridi kali yeye na kachanga kake aliko kuwa nako.Mama yangu hakuwa mzee sana lakini alikuwa na maisha magumu tu na alioneka sio wa kisasa kutokana na vitenge vilivyo chanika alivyo kuwa akivaa na miangaiko ya juani alio kuwa akifanya kutafuta riziki.Mama alichukia wanaume  wanao kunywa pombe maana alihisi wote ni sawa.

Baada ya miaka mitatu mama akajitahid akawa amepanga chumba ingawa alikuwa bado na maisha magumu.mama alipo pata chumba akatamani kunifata maana alijua nateseka kukaa na mama wa kambo.Mama alikuja mchana akaniita “mwanangu njoo” nilipo muona mama nilifurah na kumkimbilia alisema nimekufata tuondoke sikukataa maana mateso ya nyumbani nilikuwa nayajua.
Kipindi tunaondoka bahati mbaya tulikutana na baba njiani akasema; “we mwanamke unampeleka wapi mwanangu” mama akajibu, nimemfata mwanangu nikaishi nae mwenyewe ona alivyo konda chakula hamumpi nimekuta anafanya kazi ngumu sana mtoto.

Baba akasema “hakuna kuondoka na mtoto mama alianza kulia nililia pia maana baba alimpiga kofi mama, mama hakuwa na jinsi aliniacha na¬† akarudi peke yake.
Baba akufurahi kumuona mama akianza kupendeza ndo akaenda kazini kwa mama akamuita bosi wake mama kisha akaanza kumpa maneno ya uongo kuwa.. “huyu ni mke wangu, nimemfukuza kwangu sababu alitaka kuniua na sumu na anatoka katika familia ya kichawi kwahiyo kuwa makini nae atakuulia wateja”

Baada ya baba kuondoka bosi wa mama aliogopa hivyo akamsimamisha kazi mama, mama alimbembeleza bosi wake amsamee lakini alikataa akasema “rudi kwa mmeo”.
Baada ya miezi miwili kuisha mama alishindwa cha kufanya maana kodi ya nyumba ilikuwa imeisha na alikuwa hana ata senti.Ndipo aliamua kumkubalia kimahusiano japheti, ingawa japheti alikuwa anakunywa pombe pia yani kumshinda ata baba.Waliishi kama miezi mitano bila ugomvi mpaka mama upendo ukawa mkubwa kwa japheti.Ila Baba alipo mgundua japheti.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here