SHARE

SEHEMU YA 3.

Baba alipo gundua kuwa mama anatembea na japheti, hakufurahi ila alifurahia pale mama alipo kuwa akiteseka na kunyanyasika.Alimfata japheti na kumwambia, “japheti nakuomba uachane na mke wangu,tena nisikuone nae maana itakuwa ugonvi mkubwa na  mmoja wetu kuvuja damu kabisa, nitakuua kwa mikono yangu miwili.”Japheti alikuwa muoga sana ndipo akajibu “sawa nimekuelewa nimemuacha mkeo”.Japheth alipo fika nyumbani hakutaka ata kuongea na mama! Mama akamuuliza “japheti mme wangu tatizo nini? Mbona umebadilika leo? Naomba unijibu japhe!” Japheti alikaa kimya bila kuongea ila mama alikuwa ni mwanamke anae jali sana, alimsogelea japheti akamuuliza huku  akimpapasa mikononi akasema “mme wangu nakutegemea sana wewe japheti kama unavyo jua sina mama sina baba na sina msaada wowote kwahiyo ukikaa kimya nakosa raha”.

Japheti akajibu kwa asila “kwahiyo mimi ndo msaada wakati unataka kuniua na mmeo, kumbe nyie bado mnamahusiano ebu niache”Japheti alimsukuma mama pembeni akasema “sikutaki tena we mwanamke” mama alilia kama mtoto mpaka mafua yakamtoka maana alikuwa tayali anampenda japheti.
Japheti alichukua begi na godoro akaondoka mama alilia zaidi akisema “niachie godoro japheti nitalalaje na mwanangu leo”Japheti hakusikia akaendelea kutoka nje maana godoro  alilinunua kwa pesa yake, mama aliendelea kulia kwa nguvu akisema kwa machozi “jamani japheti rudisha godoro” kipindi mama analia kulikuwa na wananchi wenye asila kali walihisi japheti ni mwizi wa godoro ndipo wakaanza kumpiga bila kujua .

Japheti alilia nakusema sijaiba niacheni ila hawakusikia waliendelea kumshambulia
Mama pia alilia akisema huyo sio mwizi ila sauti ya mama ilikuwa ndogo hivyo alikuwa hasikiki.
Japheti alipigwa sana maana alirushiwa wame na kupigwa na miti kichwani. sababu watu walikuwa wanachukia wezi ule mtaa hivyo basi mwizi asinge pona kama akikamatwa.

Kutokana na japhe kupigwa sana masikini kaka wawatu alifariki! sura  ikiwa haitamaniki.
Mama alilia sana , japhe alibebwa na alizikwa na police maana hakukua na wakumzika.
mama alikata tamaa kabisa na maisha!Aliugua sana ila hakuwa na msaada wa dawa na chakula baba alikataa kumsaidia  mama. Baada ya siku mbili mtoto wake pia akaugua.

SEHEMU YA 4.

Mtoto wa mama aliugua sana tena alikonda mno maana alikuwa apati chakula wala dawa mule ndani, sababu mama pia alikuwa anaumwa zaidi hivyo wote walikuwa awana nguvu sababu ya ugonjwa, hali ya mtoto iliendelea kuwa mbaya! ndipo mama akakojoa na kumnywesha mtoto mkojo wake!  kuona kama labda  mwanae atapata nafuu au afadhali kidogo sababu hakukuwa na msaada wowote wa chakula au dawa mule ndani mama alisema “kweli masikini atabaki kuwa masikini na tajiri atabaki kuwa tajiri” mama alikuwa anampenda sana mwanae hivyo akaamua kujikaza kimalikia na kutoka nje kuangalia kama anaweza kupata chakula ili mwanae asife.

Mama Alienda chumba cha jirani yake maana mda mwingi walikuwa wakicheka pamoja nae; mama akamwambia “mama jesca ninaumwa sana mama, Mwanangu pia ana hali mbaya naomba unisaidie chakula tu leo ili ninusuru uhai wa mwanangu na mimi maana ninanjaa sana mama jesca”.
Mama jesca akajibu “hahahaha nitokeee uko! uliambiwa hapa ni kituo cha watoto yatima sikia sasa nikwambie we mchawi ulieshindwa kuishi na mumeo chakula ninacho lakini sikupi” mama aliumia. ndipo wakati anajivuta akinyata kwenda kwa baba ili amuelezee labda angeweza kumsaidia, alikutana na kijana mmoja anaitwa HANS; Hans alipita tu akiwa anaendesha baisikeli yake akamuuliza mama. “we mama mbona unatembea kinyonye hivyo barabarani tena mwenyewe tatizo nini?” Mama akamuelezea hali ya maisha na jinsi mtoto anavyo umwa ndipo HANS alipatwa huruma akanunua chakula na kumwambia twende tukamchukue mtoto ili tumpeleke hospitali.

Mama alifurahi nakusema “kweli mtu anaekusaidia ni usie mjua”. Hans aliwachukua wote na kuwapeleka hospital walitibiwa wote mtoto akapona na akapata nguvu kabisa lakini ugonjwa wa mama ulishindikana hivyo aliitajika kupelekwa nje ya nchi tena kabla ya siku mbili, mama alikata tamaa sababu zile  galama za nje hakuna ambae angeweza kuzilipa, Akamwambia HANS kuwa “kaka nakushukuru msaada wako ingawa sitapona ila mwanangu amepona naomba umtunze mtoto maana nayeye ni yatima kama mimi akikua umwambie nilibakwa na watu nisio wajua ndipo nikapa mimba yake na ana kaka yake” kweli hazikupita ata siku mbili mama akafariki


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here