SHARE

Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu ya soka nchini England,Chelsea leo jioni watakuwa nyumbani Stamford Bridge kuanza safari ngumu na ndefu ya kuutetea ubingwa wao kwa kucheza na Burnley bila ya nyota wao,Pedro anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
Pedro mwenye umri wa miaka 28 ameripotiwa kuwa hataonekana dimbani leo kutokana na kushindwa kupona kwa wakati jeraha hilo alilolipata Jumapili iliyopita kwenye mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Arsenal ulioisha kwa Chelsea kufungwa kwa penati 4-1 baada ya sare ya bao 1-1.
Mbali ya Pedro pia Chelsea itamkosa winga wake,Victor Moses ambaye anaanza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata mwezi Mei kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Arsenal.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here