SHARE

SEHEMU YA 5.

Mama alipo tangulia mbele za haki, baba alipigwa simu na watu ambao walikuwa wameisha pata taarifa kuusu kifo cha mama wakimsihi baba aweze kuhudhulia kwenye mazishi ya mama yani wote baba pamoja na mimi mwanae. Lakini tulimshanga sana baba alivyo sema! “Siwezi kuja kwenye msiba wa huyo mwanamke tena mimi huyo mwanamke simtambui kabisa msiniusishe kwa chochote kile tafadhali nawaomba”walimjibu baba na kusema kwamba, “sikiliza kaka huyu mwanamke ni yatima hana mzazi yoyote yule na wewe na yeye mliishi kwa mda mrefu sana tena vizuri bila ugomvi!

Tena yani ni mzazi mwenzako! maana mmezaa mtoto! kwanini unamkataa sahiv jamani” Baba alikata simu palepale. Mimi nililia nakusema; baba nataka kumzika mama, lakini baba alinigombeza na kusema “hakuna kwenda mahala popote utabaki ndani tu leo ”
Mama wa kambo alikuwa na roho mbaya lakini ata yeye hili swala lilimgusa akamwambia baba “Mme wangu ungempeleka mtoto na wewe pia mkamzike marehemu sio vizuri tukamtelekeza na tunamjua”.Baba alijibu nakusema “mke wangu yani tangia nimekupata wewe na nimeishi na wewe humu ndani sijawai kufikilia mtu yoyote yule ata wazazi wangu sijawai kabisa, nakupenda sana mke wangu! kila mda nakuwaza wewe na kukusikiliza usemacho nakupenda wewe tu, kwahiyo nikitoka hapa nikaenda msibani ni dhahili kuwa sikupendi sasa sitaki tena kusikia hayo mambo ya kuzika, kwan mlitaka nani afe nisimzike acheni kunisumbua akha!”

Mama alizikwa kwenye makabuli ya wilaya bila ndugu yoyote kuwepo, na ghalama za mazishi ni kwa michango ya pesa iliyo patikana kwenye rambirambi baada ya daftali yenye picha ya mama  kutembezwa barabarani.Watu walisikitika sana kitendo alicho fanya baba cha kumkana mama!Wengine walisema, “jaman mwanaume huyu ana roho mbaya sana sio mtu wa mungu kabisa.

Wengine walisema kwamba “mke wake wa pili anatabia za kishirikina ndo kamgeuza akili mpaka kamsahau mkewe! maana sasa hiv huyu mwanaume ata mama ake mzazi hamsaidii chochote kile yupo anaangaika tu lakini mkewe anapendeza sana wakati kipindi marehemu yupo aliwajali wazazi wake ndugu zake ata sisi rafiki zake alitukumbuka lakini tangu abadilishwe akili anatuzalau wote tusimlaumu maana damu yake imechezewa.

SEHEMU YA 6.

Jamii yote iliyokuwa imetuzunguka ilimshangaa sana baba kwa kitendo cha ajabu kisichofaa alichokuwa amefanya cha kumtelekeza mama! Lakini baba akuwa na wasiwasi wowote ule alihisi yupo sahihi. Ilipo pita miezi miwili maneno  mataani kuhusu kifo cha mama yakawa yamekatika mama akaanza kusaulika.
Kesho yake siku ya jumanne baba alipigiwa simu na rafiki yake! akamwambia kuwa kunakazi nzuri sana mkoani ya uchimbaji wa madini mgodini baba aende wakafanye maana ilikuwa ina lipa! Baba alikataa akasema siwezi kuja uko nikamuacha mke wangu peke yake ata kama pesa hipo.

ila mama wa kambo alimwambia baba kuwa, “mme wangu tusichezee kazi maana ni kazi kupata kazi, naomba tu uende ukatafute pesa tuishi maisha mazuri zaid” Baba alikubali ndipo akaanza kujiandaa ili aweze kwenda mkoani kwenye migodi  kusimamia uchimbaji wa madini ili  kutafuta pesa za kutosha. Wakati baba anajiandaa alishangaa kuona naanza kulia akauliza, “mwanangu unalia nini”? Nikajibu nikitoa machozi, “baba unaondoka unaniacha,” Huku machozi  yanatoka nalia nikikohoa bila hata kuwa na kikohozi tena  mbele ya mama wa kambo.

Nililia sababu nilikuwa najua nitateseka pale nyumbani maana mke wa baba alikuwa hanipendi kabisa! Baba alipo maliza kujiandaa mimi na mama wote tulimsindikiza stendi ya basi aweze kusafili, tulipo rudi nyumbani mimi na mama kabla ata sijakaa kwenye kochi sebleni nilipigwa kofi pah Mgongoni nilianguka chini maana sikutegemea kofi, nilishtuliwa nikahisi ni shoti ya umeme mama akasema “kilicho kuwa kinakuliza kisa baba ako anaondoka ni nini? inamaana hunipendi sio? Kesho hakuna kwenda shule amka mapema deki nyumba na choo osha vyombo vyote na unipikie chai” nililia sana nikasema sawa mama, niliamka mapema nikafanya kama nilivyo ambiwa maana nilimuogopa sana mama angenipiga sana nisipo msikiliza, siku moja aliniita akasema “nampigia baba ako simu akiuliza unaumwa sema ndiyo ili anitumie pesa mimi” baba alipo niuliza nilikubali kwa shinikizo tu maana ningepigwa!Siku moja nipo nje ninalia mgeni wa mama alikuja akanikuta nalia akaniuliza mbona unalia nikasema mama ameninyima chakula, mgeni akaguna  alipo ingia ndani akakuta mama anakula vyakula peke yake na juisi. Akasema “kha!!”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here