SHARE

Kocha Joseph Omog amesema wazi kwamba mpaka sasa anakoshwa na aina ya upambanaji wa Erasto Nyoni na Shiza Kichuya

 Kocha mkuu wa klabu ya Simba Mkameruni, Joseph Omog amekoshwa sana na hali ya upambanaji wa Erasto Nyoni pamoja na Shiza Kichuya kwa jinsi wanavyojituma.

Akifanya mahojiano na Mwanaspoti, Omog amesema kuwa ana wachezaji wenye majina makubwa kwenye ligi na walifanya vizuri, lakini ndani ya Simba hata angalia ukubwa wa majina, na atatoa nafasi kwa wale watakaokuwa na moyo wa kujituma na hamu ya ushindi kama ilivyo kwa Nyoni na Kichuya.

“Mpaka sasa hali siyo mbaya wachezaji wanajituma kwa nafasi yao, watu kama Kichuya na Nyoni ndiyo mfano mzuri wa aina ya kupambana ninayoimaanisha.”

“Kila mchezaji moyoni mwake atambue anatakiwa kupambana, (Huku anapiga ngumi kwa mikono yote miwili) muda wote, kama tukishinda siyo mabao mawili matatu watu wanaridhika, kama ni kufunga tunatakiwa kufunga mengi tu,” alisema Omog.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here