SHARE

Mabingwa mara tatu mfululizo na mara 27 kwenye historia ya soka nchini Tanzania timu ya Yanga Sc imepoteza mchezo wa kirafiki jioni ya leo baada ya kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ alimfunga kwa kichwa cha mkizi kipa wake, Ramadhan Kabwili dakika ya 22 wakati akijaribu kuokoa krosi ya Shalla Juma kutoka upande wa kushoto wa Uwanja kuipatia bao pekee la ushindi Ruvu.

Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima nguvu kwa Yanga inayofundishwa na kocha Mzambia, George Lwandamina baada ya Jumamosi iliyopita kushinda 3-2 dhidi yas Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na baada ya matokeo hayo, Yanga SC itaondoka Dar es Salaam mapema kesho kwenda Zanzibar ambako usiku watamenyana na Mlandege Uwanja wa Amaan katika mchezo mwingine wa kirafiki.

Mapema Jumatatu Yanga watakwenda kisiwani Pemba kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba Agosti 23 Uwanja wa Taifa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here