SHARE

Timu ya soka Real Madrid imefanikiwa kuituliza akili ya kiungo wake mahiri,Francisco Román Alarcón Suárez maarufu Isco baada ya kumsainisha kandarasi mpya ya miaka minne ya kuendelea kusalia Santiago Bernabeu.
Isco ambaye mkataba wake wa sasa ulikuwa unaelekea ukingoni ameripotiwa kusaini kandarasi hiyo mpya hivi karibuni na kuzima uwezekano wa kuihama klabu hiyo na kujiunga na Barcelona ambayo ilionyesha nia kumtaka kumsajili.
Katika kandarasi hiyo mpya,Isco mwenye umri wa miaka 25 atakuwa akilipwa mshahara wa kiasi cha Euro Milioni 6 kwa mwaka na kuingia kwenye orodha ya mastaa wanaolipwa vizuri Santiago Bernabeu.
Pia kandarasi hiyo mpya ina kipengele kinachosema klabu yoyote ile itakayomtaka kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania itoe dau la Euro Milioni 700.
Dau hilo ni mara tatu zaidi ya dau la Euro Milioni 222 ambalo limetolewa hivi karibu na matajiri wa soka la Ufaransa,PSG kumsajili staa wa Brazil,Neymar kutoka Barcelona.
Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kwa sasa hakuna mchezaji yoyote yule kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid ambaye kwenye mkataba wake ana kipengele cha mauzo ya chini ya Euro Milioni 500.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here