SHARE

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es salaam, imetenga kiasi cha sh. bilioni 1.5 kwaajili ya vikundi vya vijana na wanawake.

Hayo yameelezwa  na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Benjamin Sitta wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Kawe.

 

Meya Sitta amesema, kiasi hicho cha fedha kitatolewa kwa njia ya mikopo ya riba nafuu zaidi kama sera ya serikali inavyoelekeza, huku utaratabu wa kupata mikopo hiyo utaanzia katika
ofisi za seirikali za mitaa.

“Mikopo itatolewa kwa vikundi vyote vilivyo sajiliwa, nawataka
wananchi wa Kinondoni kuonana na maofisa utamaduni ili kupata
utaratibu wa kupata fedha hizo “alisema Meya Sitta.

Wakati huohuo Meya huyo amesema ametangaza ujenzi wa stendi ya kisasa ya daladala katika eneo kawe, Ujenzi wa stendi hiyo utasaidia kuondoa kero ya msongamano bara barabarani.

“Tutajenga stendi kubwa eneo la Mzimuni, Itakuwa na mabanda ya wafanyabiashara hivyo itakuwa ni fursa kwa wananchi kujipatia kipato” alisema Meya Sitta.


Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo wameoneshwa kufurahishwa na ahadi alizotoa Mstahiki Meya Sitta kwani kero ya stendi na suala la hali ngumu maisha lilikuwa likiwatatiza kwa muda mrefu, lakini Mstahiki Meya amewaletea matuamaini mapya.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here