SHARE

Msanii mkongwe wa muziki wa hiphop nchini, Dudu Baya ameendelea kupigilia msumari kauli yake ya kwamba Nay wa Mitego sio mc na hawezi kujilinganisha na wakina Godzilla na Nikki Mbishi

Dudu baya amesema hayo huku akidai kwamba uandishi wa Nay ni kama wa Gigy Money kwani hauna maana yeyote zaidi ya kutaja taja majina tu .

“Mimi nilizungumzia kwamba nay wa mitego sio Mc asiingie kwenye ile dunia ya kina nikkimbishi, wakazimusic, Kingzilla_tz wale aachane nao wale ni ma’MC yeye kashazoea kuwaimba imba Bongo Movie. Uandishi wa Nay wa Mitego ni sawa sawa tu na wa Gigy_money_og au Amber___lulu kwasababu uandishi wa Nay ni kutaja taja tu majina ya watu maarufu na nyimbo za hivyo mimi naandika hata mia kwa lisaa limoja” alisema Dudubaya

Speaking of uandishi wa naytrueboy wa kutaja taja majina ya watu maarufu, Dudubaya ni mmoja kati ya wasanii waliotaja kwenye track ya nay ‘Itafahamika’ ambapo rapper huyo alipita na mstariĀ  Dudubaya kawa mganga, Mr Nice anauza shanga’


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here