SHARE

SEHEMU YA 13.

Yule mwanamke alikuja amekasilika sana anataka kumuua mama na kisu, maana alionyesha kuwa na wivu kwa mmewe. Kipindi mama yupo na yule mwanaume walisahau kufunga  mlango walipo ingia chumbani wakadondoshana moja kwa moja mpaka kitandani, mama alikuwa huru sana Maana ile miezi baba angu alikuwa amesafili kikazi hivyo mama alikuwa anatumia pesa za baba kumpata kila mwanaume alie mpenda! Na mama alipenda sana vijana wadogo wadogo maana babay angu umli wake ulikuwa tayali umeenda.

 

Yule kaka akasema kwa mama “mpenzi funga mlango kwanza” lakini mama akawa kapagawa tayali na yule kaka mpaka akapatwa na uvivu wa kuufunga malango! akasema, “achana na mlango mpenzi wangu naomba raha tu” kipindi wameisha vua nguo wamebaki na nguo za ndani peke yake,  walishangaa ghafla mlango unagongwa na yule mwanamke akisema”fungua mlango” yule kaka akaogopa sana maana alisikia sauti ya mkewe! Mama akauliza “tatizo nini” yule kaka akasema “huyo ni mke wangu maana sauti kama yake” wote walianza kuogopa!Mama akauliza “nani tena kamwambia sisi tupo huku?” Aliendelea kugonga akisema “fungua” kipindi anagonga mlango kwa hasila  Mlango ukafunguka maana walikuwa hawajaufunga mlango kabisa kipindi wanaingia. Yule mwanamke akasema “mme wangu tabia gani hizi upo uchi na huyu malaya unaniacha ndani sijala naangaika na watoto?”

 

Mama alipo ona kisu akakimbia nje akiwa amevaa nguo ya ndani tu! Yule dada akamfata akisema we malaya lazima nikuue! mme wake alikuwa muoga sana alikimbia akawaacha mama na mke wake, yule mwanamke alipo taka kumchoma kisu mama, mimi nilikuwa maeneo yale yale  nilimuonea huruma sana mama nilimfata karibu kipindi anataka kumchoma tumboni, nikakinga mkono wangu wa kushoto, kisu kikanichoma mimi,kipindi ninalia maumivu ya kisu mama alinishangaa sana maana alijua bado nipo kituo cha police nimefungwa! Alikimbia kwa uoga maana aliona haibu nimemtazama akiwa uchi! Alikimbia uchi kila mtu mtaani akimshangaa! akaniacha nikiwa nalia sana pale; maana maumivu yalikuwa makali mkononi, ila yule mwanamke akanionea huruma kisha akanibeba na kunipeleka kwake kumbe pale kwake ndipo palikuwa kwa HANS alie msaidia mama na mdogo wangu wa kike! lakini mimi sikujua kama pale kuna mdogo wangu!

SEHEMU YA 14

Nilipo fika kwa yule mama niliwaona watoto wake wote ila nilipo muona mdogo wangu tu dahh! moyo wangu ulishtuka nikahisi nywere zinasisimka kabisa, Sikuelewa  pale pale kama ni mdogo wangu hivyo nikatulia tu.
Nilitibiwa na kupona vizuri, baada ya week moja yule mama akaniuliza kuhusu familia yangu na kwanini nafanya kazi za kuokota makopo na vyuma wakati natakiwa kuwa shule sababu umli wangu unaruhusu.

Nilimuelezea kuwa “mama angu alifukuzwa na baba angu nyumbani nikiwa mdogo sana; na baba akaoa mwanamke mwingine nyumbani, mama aliteseka mpaka alifariki dunia nikiwa mdogo sana, Hivyo nimeishi na mama wa kambo kwa mda mrefu na amekua akinitesa; na kumfanyia baba mzazi vitu vibaya sana kama kulala na vijana wadogo kwake, sio hivyo tu bali yeye pia alichezea “damu ya baba” nikiwa naona kwa macho yangu hivyo baba angu anamsikiliza tu mama na hanisaidii chochote mimi alinifunga polisi! Eti kisa nimemwambia kuwa mama ni mchawi! Ila police nikatoroka mpaka sasa sina pa kula wala pa kulala wewe ndo msaada wangu” yule mama akasema dah! wanawake wengine wanaroho mbaya sana sijui uyo mwanamke yukoje jamani? Nilimjibu na kumwambia kuwa “ni yule ulie taka kumchoma kisu nikatega mkono wangu kumnusulu maisha na uhai wake! Dah! Kwanza alishtuka akajibu “jamani we mtoto una roho nzuri sijapata kuona yani umemuokoa huyo mama wakati amekufanyia ubaya” nilimjibu “hiyo yote ni mipango ya mungu” Baada ya mda mme wake akawa amefika, Mr Hans alipiga magoti chini akamuomba mke wake msamaha; kweli mke wake alimsamee!

lakini mimi kila nilipo kua namuona mdogo wangu, nilikuwa najisikia tofauti mwilini mwangu, kumbe damu nzito kuliko maji.
Watu walishangaa sana kile kipindi  maana mke wa baba alikuwa atoki ndani, kwa zile aibu za kukimbia uchi kutoka gesti baada ya kufumaniwa na mme wa mtu; ndugu na majirani ambao hawakuwepo gesiti walizani kuwa labda amechanganyikiwa mpaka kuonyesha mwili wake waziwazi, walienda kwa mama kumjulia hali lakini mama aligoma kabisa  kufungua mlango ndipo wakampigia simu baba lakini baba ila akawatukana; dah usiku kila mtu akaondoka.
Usiku huohuo nikiwa nimelala nikaota kuwa..

Usikose sehemu ya 15


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here