SHARE

Nyota wa Liverpool Roberto Firmino amekiri kuwa litakuwa pigo kwa Liverpool ikiwa Philippe Coutinho ataihama klabu hiyo.

Kiungo huyo inaaminika ametoa maombi ya kutaka kuondoka kupitia barua pepe baada ya kuielewa nia ya Barcelona.

Miamba wa Catalan, ambao wamemuuza Neymar kwa ada inayokadiriwa kuwa paundi milioni 200, imeripotiwa ofa yao ya paundi milioni 72 kwa ajili ya Coutinho ilikataliwa na ofa nyingine inayokadiriwa kuwa paundi milioni 80 ilikataliwa pia.

Mchezaji huyo, 25, alikosa mechi ya Jumamosi Ligi ya Uingereza Liverpool wakianza kwa sare ya 3-3 dhidi ya Watford kutokana na majeraha ya mgongo, na hakusafiri kwa ajili ya mechi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa dhidi ya Hoffenheim.

Akaunti ya twitte @BrazilStat ilimnukuu Firminho akisema: “Sitaki kufikiri [kuondoka kwa Coutinho] kwa sababu itakuwa ni pigo. Ni mchezaji mahiri lakini pia rafiki yangu.”

Mchezaji huyo wa zamani wa Milan, aliyejiunga na Liverpool 2013, alikuwa mshenga wa arusi ya Firmino mapema msimu huu wa majira ya joto.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here