SHARE

Mjamaica Usain Bolt alikuwa nchini Uingereza katika mbio zake za mwisho kabla ya kustaafu, Bolt alikuwa akishiriki michuano ya World Championship ambapo hata hivyo haikuisha salama kwake.

Jumamosi iliyopita Bolt alipata majeraha baada ya kuumia wakati akiwa katika mbio za 4 × 100 mjini London akiwa anajaribu kutafuta medali yake ya mwisho ya dhahabu kabla ya kustaafu.

Majeraha ya Usain Bolt yamekuja ikiwa imebaki siku kadhaa kufika mwezi ujao ambako kutakuwa na mchezo wa kuchangia jamii kati ya wakongwe wa Manchester United na Barcelona.

Mchezo huu ulikuwa nafasi ya pekee kwa Bolt kuichezea United kwani mara kwa mara amekuwa akisema ana ndotobza siku moja kuichezea United ambayo ndio timu yake kipenzi.

Kupitia Twitter Bolt aliweka picha za jeraha lake na aliandika “sijawahi kuweka hadharani kuhusu matibabu yangu, lakini hii ni kwa sababu mumekuwa mukiuliza kama nimeumia kweli au hapana, nimeumia na siwezi kuwadanganya”

“Asanteni sana kwa kunipa ushirikiano mashabiki zangi na sasa inabidi nipumzike ma kuendelea na masuala mengine ya maisha yangu” alimalizia Bolt kwa kuwashukuru mashabiki zake.

Wakongwe mbalimbali kama vile Phill Neville, Edwin Van Der Sar, Paul Scholes, Wes Brown na wengineo watakuwepo uwanjani tarehe 2 mwezi ujao kukipiga dhidi ya wakongwe wa Barcelona.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here