SHARE

Siku chache baada ya kuenea kwa madai kuwa mume wa ndoa wa mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel, Sunday Demonte ameachiwa huru huko Dubai baada ya kutumikia kifungo cha miaka kadhaa huku staa huyo akishi kinyumba na mwanaume mwingine, muigizaji huyo amesema ndoa hiyo haipo tena.

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Aunt ambaye alifunga ndoa na Demonte yapata miaka minne iliyopita, alisema kuwa, anawashangaa watu wanaoikomalia ishu hiyo ambayo kwa upande wake ni ndogo.

Ngoja niulize, hivi jamani mbona watu siyo waelewa? Nani asiyejua kama mimi niko na mtu hivi sasa?

Na ninaamini kabisa hata yeye (Demonte) anajua? Kwa hiyo hata kama ameachiwa huru na akaja, ukweli utabaki kuwa ndiyo huohuo tu, kwamba tayari nina mtu mwingine maana hata yeye asingeweza kusubiri muda wote huo, hivyo ajue tu hana chake,” alisema Aunt.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa hivi sasa ni vigumu kuachana na mzazi mwenziye aliyenaye kwa kuwa tayari wana mtoto ambaye anapenda kuwaona wakiwa pamoja, hivyo hawezi kumtesa mwanaye.

Hebu fikiria, mtoto wangu amezoea kutuona pamoja mimi na baba yake na ni kitu ambacho anakipenda sana, sasa kwa nini nimuumize?” alihoji Aunt.

Risasi Mchanganyiko baada ya kuzungumza na Aunt, lilimtafuta mzazi mwenziye huyo ili azungumzie ujio wa mume wa ndoa wa mpenzi wake, lakini alisema yeye hana cha kuzungumza, isipokuwa mwenye uamuzi wowote ni Aunt.

Unajua kwenye jambo kama hilo mtu anayeweza kuzungumza vizuri ni Aunt mwenyewe na yeye ndiye mwenye uamuzi wote, ninachojua mimi ni baba mtoto na itabaki kuwa hivyo siku zote,” alisema kijana huyo.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here