SHARE

Shemeji yake alimwambia mama akafungue mlango maana yeye tayali alikuwa kaisha ogopa,
yule dada aliingia ndani akiwa analia sana masikini, mpaka kamasi linamtoka puani kabisa kwa maumivu na uchungu “hama kweli mume wa mtu mchungu” yule dada akasema “rafiki yangu fadhila zote zile, leo unanilipa hivi”.

Akamwambia na mme wake “mme wangu hii ndiyo ahadi yetu tulio peana kanisani sio?ya kulala na mwanamke tena mbaya zaidi kwenye kitanda changu” Huku akiwa analia sana dada wawatu mpaka macho yakabadilika rangi na kuwa mekundu.
Mama yangu alianza kulia akisema “nisamee rafiki yangu sirudii tena kuja chumbani kwako rafiki yangu nisamee shetani na ibilisi kanipitia” Mme wake akasema “mke wangu hatujafanya chochote kibaya nilikuwa namwambia aniandalie chakula maana leo nimewai kutoka kazini nilijihisi mchovu! nisamee sikukupa taarifa mke wangu.

Yule dada alimpiga kofi chungu sana mme wake! akamwambia ebu angalia hiyo nguo ya ndani uliyo vaa kama ni yako.
Mme wake alivyo jitazama alikuwa hajafunga taulo vizuri na alikuwa amevaa nguo ya ndani ya mama!
kilicho mchanganya ni langi maana zote zilikuwa nyeupe
Na walivaa nguo haraka haraka kwa huoga kuwa wamekamatwa,
mama na yeye alivyo jitazama akakuta amevaa nguo ya ndani ya shemeji yake.

Yule dada machozi yanamtoka akamwambia mme wake “utamuitaje huyu mwanamke ndani akiwa amevaa utupu hivi. Nyie hamjaanza leo mmeanza zamani leo nashukuru mola kanionyesha waziwazi”.
Yule dada alikuwa na roho ya huruma sana alimwambia yule mwanamke “Sina cha kukufanya maana tayali umeisha tembea na mume wangu nacho omba chukua nguo zako na kila kitu chako uondoke”
Mama alipiga magoti akasema “nisamee rafiki yangu mme wako alinilazimisha sana mpaka nikajikuta nashawishika sirudii tena rafiki yangu!

Dada akasema..Mme wangu huyu mwanamke nilimkuta sehemu amebakwa! tena mbaya zaidi alibakwa na vijana tisa wa mtaani, nilipo muona hana sehemu ya kuishi nikaona ni bora tukae nae wote hapa! Sasa wewe umetembea nae! una uwakika gani kama ni mzima ki afya na nimekutazama ata kinga hujatumia wewe unasaliti ndoa tu,  Mme wake akasema…nisamee mke wangu nakuhaidi siwezi kurudia hivi tena.
Mama akasema nisamee pia rafiki yangu..
Usikose sehemu ya #32


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here