SHARE

Mambo yanazidi kuwa mambo! Lile saga la mwanamitindo wa kitaifa na kimataifa, Hamisa Hassan Mobeto, kudaiwa kuzaa na msanii wa bongo Fleva linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha, nyuma yake kukiwa na sarakasi nyingi ambazo siyo za nchi hii.

Ubuyu mpya mjini unadai kwamba, staa mwenye jina kubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu amejitosa kwenye sakata hilo akidaiwa kuungana na mpenzi wa sasa wa Wema, Zari… msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa ajili ya kumbutua Hamisa kwa kuwa jamaa huyo pia aliwahi kuwa mpenzi wa Wema (x boyfriend wake).

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Wema, baada ya Hamisa kutikisa kwa ishu hiyo na kuungwa mkono na Wabongo wengi huku Zari akibaki peke yake, Wema na timu yake (Team Wema), wanadaiwa kuungana na Zari kwa ajili ya kumsaidia kujibu mashambulizi mitandaoni.

“Yaani kila kukicha mambo yanazidi kupamba moto kwenye mitandao ya kijamii. Unajua Zari alikuwa anashambuliwa kama mpira wa kona na wengine walikuwa wakimponda Wema kuwa alishindwa kuzaa na jamaa huyo ‘so’ Hamisa amempiga bao. Sasa Wema alichukizwa na watu wanaomsema vibaya wakimhusisha na tukio la Hamisa kuzaa na msanii huyo.

“Unaambiwa ghafla Wema amekuwa akionesha chuki za waziwazi anapoona au kuonesha habari inayomsifia Hamisa kuzaa na jamaa huyo.

“Na kweli upepo umeanza kubadilika maana Zari naye ameanza kupata sapoti ya kumshambulia Hamisa kutoka kwa Team Wema,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Wema na kumuuliza juu ya yeye na timu yake kuungana na Zari katika kumshambulia Hamisa ambapo katika hali ya kushangaza, mwanadada huyo alikiri kumchukia Hamisa bila kutaja sababu.

Wema alisema kuwa, huko nyuma alikuwa na mapenzi makubwa kwa Hamisa, lakini hivi karibuni amejikuta tu hampendi.

“Nimekuwa simpendi tena kabisa na hata sasa hivi ukiniuliza sababu, siwezi kukujibu ni kwa nini simpendi.

“Huko nyuma nilikuwa ninampenda, lakini katika hali ya kawaida, simpendi tena,” alisema Wema. Hamisa anadaiwa kuzaa na msanii huyo ambaye amezaa na Zari watoto wawili kabla ya kusemekana kumtelekeza huku wazazi wa jamaa huyo wakipokea baraka hiyo kwa mikono miwili.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here