SHARE

Kesi iliyofunguliwa na muungano wa NASA ya kupinga matokeo ya Uchaguzi MKuu wa Novemba 8 nchini Kenya imeanza kusikilizwa leo na Mahakama Kuu ya nchi hiyo.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) mkuu wake Wafula Chebukati, muungano wa NASA na Rais Uhuru Kenyatta wametakiwa kuwasilisha mashtaka na utetezi wao.
Chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta kimewasilisha mambo matano ya kuzingatiwa mahakamani huku muungano wa NASA ukiwasilisha masuala 28.
Masuala yaliyowasilishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ni mawili.

Raila Odinga, mkuu wa muungano wa NASA

Shauri hilo ni la kutoa maamuzi kuhusiana na iwapo Rais Uhuru Kenyatta amechaguliwa kisheria na kutangazwa mshindi kwa njia sahihi au la. Hukumu ya Mahakama Kuu ya Kenya inasubiriwa kwa shauku kubwa kuhusu suala hilo.

Kabla ya hapo Kiongozi wa Muungano wa NASA, Raila Odinga alikuwa amesema kuwa, matokeo ya uchaguzi yaliyokusanywa kutoka vituo vya kupigia kura zaidi ya theluthi moja yalichachakuliwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwepo kwa kasoro katika mfumo kielektroniki uliotumika kusambaza makaratasi ya matokeo ya kura.

Hata hivyo IEBC imekanusha madai hayo na tayari imewasilisha fomu zilizotumika kukusanya matokeo hayo ikisema ni safi na hazina matatizo yoyote.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here