SHARE

Manchester City wanataka kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kabla ya dirisha la kuhama wachezaji kufungwa Alhamisi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alifungia Arsenal mabao 24 Ligi ya Premia msimu uliopita lakini mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Bado hajatia saini mkataba mpya Emirates.

Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili.

before Thursday’s transfer deadline.

Meneja wa City Pep Guardiola inadaiwa anataka kumnunua Sanchez, 28, moja kwa moja.

Hata hivyo, hatua ya kumnunua inaweza kutilia shaka mustakabali wa Raheem Sterling katika City.

Sterling, 22, anayechezea timu ya taifa ya England amechezea City mechi zao zote tatu za kwanza ligini msimu huu.

Lakini hatahakikishiwa nafasi ya kuanza mechi Etihad hasa baada ya kuwasili kwa Bernardo Silva kutoka Monaco.

BBC imefahamu kwamba Sterling anaweza kufurahia kwenda Arsenal na kurejea jijini London iwapo atakuwa kwenye sehemu ya mkataba wa kumchukua Sanchez.

Bado City hawajawasilisha rasmi ombi la kutaka kumchukua Sanchez lakini hilo linatarajiwa kufanyika wakati wowote sasa.

Sanchez alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban £35m na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here