SHARE

UGAWAJI WA MIRATHI ILIYOACHWA BILA YA KUANDIKIWA WOSIA (INTESTACY)

Kumekuwepo na mifarakano kadha wa kadha kuhusiana na ugawaji wa mirathi pale ambapo marehemu amefariki bila ya kuacha wosia. Tumeshuhudia migogoro mingi miongoni mwa wana familia kuhusiana na suala zima la kugawana mali iliyoachwa na marehemu. Katika mada ya leo tunaangalia aina za ugawaji wa mali za marehemu aliyefariki bila ya kuacha wosia.

Nini maana ya Wosia. Wosia ni maazimio yaliyo huru yanayotolewa na mtu kwa dhumuni la kutaka mali yake igawiwe kwa wahusika anaowakusudia baada ya yeye kufariki. Katika kifungu cha 2 cha Sheria ya mirathi na usimamizi wa mali sura ya 352 (The Probate and Administration of Estate Act. Cap. 352) wosia ni maadhimio yanayotolewa na mtu kipindi cha uhai wa Maisha yake bila ya kulazimishwa na mtu mwingine au bila kushinikizwa. Wosia ni lazima umuhusu binadamu na sio vinginevyo.

Ugawaji huu wa mirathi unaofanywa pale ambapo marehemu amefariki bila ya kuacha wosia unagawanywa katika makundi mawili ambayo ni (a) kufariki bila kuacha wosia na (b) kufariki wakati marehemu ameacha wosia kwa baadhi ya mali zake na mali nyingine bila kuandikiwa wosia.

  1. Kufariki bil kuacha wosia (Total intestacy)

Hii hutokea pale ambapo marehemu amefariki bila ya kuacha wosia wowote ule. Na mali za marehemu hugawiwa katika misingi ya kisheria bila ya kujali kuwa marehemu hakuacha wosia.

  1. Wosia ulioachwa kwa baadhi ya mali na mali nyingine zilizoachwa bila wosia (Partial intestacy)

Hii hutokea pale ambapo baadhi ya mali zimeandikiwa wosia na marehemu na baadhi ya mali kutokuandikiwa wosia. Katika aina hii ya wosia mali zitakazogawiwa ni zile ambazo zimeandikiwa wosia na mali ambazo hazijaandikiwa wosia zitafuata utaratibu wa kisheria ili kuweza kugawiwa bila ya kuwepo na malalamiko ya aina yoyote ile.

Katika kifungu cha 33(1) cha sheria ya mirathi na usimamizi wa mali sura ya 352 (The Probate and Administration of Estate Act Cap. 352) inaelezwa kuwa ugawaji wa mali za marehemu ambazo hazikuachiwa wosia, mhusika auwahusika wa mirathi wanatakiwa kutuma maombi mahakamani ya kumteua msimamizi wa mirathi atakaesimamia mali kwa niaba ya wafaidika wa mali ya mirathi kabla ya kuigawa kwa wahuiska kwa kuangalia misingi itakayoongoza ugawaji wa mali za marehemu.

Imeandaliwa na Ally Jumanne

allyjumanne88@gmail.com

 

 

 

 

 

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here