SHARE

Mahakama Kuu nchini Kenya, imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Raila Odinga, urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1,2017.

Mahakama Kuu ya Kenya, imefikia uamuzi huo leo Septemba 1, 2017, kufiuatia maombi ya Mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake, Bw. Raila Odinga, ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, uliompa ushindi Rais Kenyatta.

Katika maombi yake, Bw. Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matoko.

Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.

    vidokezo

  1. Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%)
  2. Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga alipata kura 6,762,224 (44.74%)
  3. Upinzani unadai mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa na kuingiliwa kumfaa Rais Kenyatta.
  4. Wakati wa kusikizwa kwa kesi, kulikuwa na mvutano kuhusu kukaguliwa kwa mitambo ya tume ya uchaguzi
  5. Mahakama ya Juu inaweza kuidhinisha au kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi.
  6. Iwapo ushindi wa Rais Kenyatta utaishinishwa, basi ataapishwa Septemba 12
  7. Iwapo uchaguzi utafutiliwa mbali, uchaguzi mwingine utafanyika katika kipindi cha siku 60.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here